Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi atengua uteuzi Kamishna Mkuu Bodi ya Mapato Zanzibar

Dk Mwinyi atengua uteuzi Kamishna Mkuu Bodi ya Mapato Z’bar

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB),  Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa  fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa Kamishna Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB),  Salum Yussuf Ali ili kupisha uchunguzi wa kina wa upotevu wa  fedha za makusanyo ya mapato zilizopotea.

Pia, ameagiza bodi ya Mamlaka hiyo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Usajili, Ukaguzi na Upelelezi wa Walipa Kodi, Hashim Kombo Haji kupisha ukaguzi wa kina wa maelekezo yake ya kuondoa taarifa za ukaguzi ambazo hatimaye hazikupelekwa kwenye bodi.

Dk Mwinyi amefikia uamuzi huo leo Februari 17, 2022 wakati akiwa katika ofisi za ZRB Mazizini ambapo amepata fursa ya kuzungumza na bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (Zaeca).

Sambamba na hayo, ameiagiza Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na watendaji waliofanya uchunguzi pamoja na kushirikiana na vikosi vyote vya ulinzi na usalama watakavyovihitaji ili kujua fedha hizo zimeendea wapi.

“Taarifa zote za kitengo cha uchunguzi lazima zichunguzwe na kufuatiliwa ili kujua ripoti zilizotolewa na kitengo hicho hatima yake ni kitu gani,” amesema

Aeagiza kufanyika uchunguzi wa lita za mafuta zenye thamani ya Sh58 milioni ili kujua ushuru wake umelipwa wapi huku akiiagiza Bodi kutokana na unyeti wa kitengo cha usajili, ukaguzi na upelelezi wa walipa kodi kijitegemee na kiwe chini ya Kamishna Mkuu.

Amesema uchunguzi uliofanywa wa moja ya Kampuni ya meli ya usafirishaji wa abiria na ilionyesha tofauti ya ulipaji wa kodi wa Sh9.65 bilioni ambazo hazikulipwa ambapo uchunguzi ulifanyika na ikaonekana kwamba muhusika kalipa lakini fedha hazikuonekana.

“Bodi ya mapato ndio moyo wa Serikali kwani ufanisi wa chombo hiki ndio unaopelekea Serikali kuweza kutekeleza majukumu yake ya kimaendeleo na uendeshaji wake,” alisema