Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi ateua vigogo akiwamo Kaimu Jaji Mkuu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi

Muktasari:

Rais wa Zanzibar na Mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa nyadhifa mbalimbali akiwamo  Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa nyadhifa mbalimbali akiwamo Kaimu Jaji Mkuu.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 20, 2021 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,, Mhandisi Zena Said  inaeleza kuwa Dk Mwinyi amemteua Jaji Khamis Ramadhan Abdalla kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu Zanzibar.

Pia amemteua Balozi Masoud Abdalla Balozi kuwa Katibu wa Rais wa Zanzibar- Ofisi ya Rais Ikulu, huku Dk Haji Mwevura Haji akiteuliwa kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Maabara ya Mkemia Mkuu.

Pia taarifa hiyo inaeleza Shaaban Hassan Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utendaji wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

“Rais awataapisha Kaimu Jaji mkuu wa Mahakamu kuu Zanzibar na Katibu wa Rais kesho Oktboa 21, 2021 saa tatu na nusu asubuhi Ikulu Zanzibar,” inaeleza sehemu ya taarifa.

“Tukio hili pia litakwenda sambamba na uapisho wa Khatib Khamis Mwadin ambaye ni Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia magendo (KMKM) aliyeteuliwa Oktoba 8 na Suleiman Abdulla Salim, Katibu wa Tume ya Utangazaji ambae aliyeteuliwa Septemba 28, 2021,