Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FCC yaja kimkakati kudhibiti bidhaa bandia

Tume ya ushindani nchini (FCC) imesema katika kuhakikisha inadhibiti uzalishaji, uagizaji, uingizaji na utumiaji bidhaa bandia imejipanga kutoa elimu kwa jamii na kuweka ulinzi imara kwenye mipaka isiyo rasmi.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 10 na Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo, William Erio wakati akielezea maadhimisho ya siku ya haki ya mtumiaji duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Machi 15 ambapo kitaifa yatafanyika jijini hapa.

Katika kilele hicho waziri wa viwanda na biashara Dk Ashatu Kijaji ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, huku kauli mbiu mwaka huu ikiwa ni Nishati safi kwa ustawi mtumiaji na mazingira.

Erio amesema katika kufikia malengo wamejipanga kutoa elimu kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kilele chake kwa wananchi na semina kwa wanafunzi katika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Mkurugenzi huyo amesema katika kufikia mipaka yote isiyo rasmi tayari wamefungua ofisi mpya mkoani Mbeya ambayo wataalamu wake watakuwa karibu kufikia maeneo yote ikiwamo mpaka wa Tunduma.

“Kwa maana hiyo kwa kushirikiana na mamlaka nyingine tutadhibiti uagizaji, uingizaji na uzalishaji bidhaa bandia na ndani ya mwezi huu ofisi itaanza kazi yote ni kuhakikisha mtumiaji anapata kilicho bora,” amesema Erio.

Amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na tume hiyo pamoja na mamala nyingine kufichua taarifa za bidhaa bandia akieleza kuwa serikali inalenga kuwa na soko lenye ushindani kwa bidhaa zote bora.

“Kwa mwaka jana malalamiko yalikuwa mengi yasiyopungua 50 japokuwa yalikuwa ya watu binafsi, hivyo tuwaombe wazalishaji kuwa na bidhaa yenye ubora kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Baadhi ya wananchi wamesema bidhaa zisizo na ubora zinachangiwa na maslahi binafsi lakini ukosefu wa elimu ya utambuzi kwa wananchi kujua bidhaa feki na halisia.

“Wafanyabiashara muda wote wanafikiria maslahi, wakikutana na mwananchi ambaye kipato chake ni cha chini na hana elimu kuhusu bidhaa bora na bandia lazima wamuuzie, wengine wanashusha hata bei,” amesema Victoria Mwasekaga.