Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FCC yashtukia washindani kula njama katika biashara

Muktasari:

  • Makundi sita wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini nchini watanufaika na elimu ya kuepuka kupanga njama baina ya washindani itakayotolewa na Tume ya Ushindani Tanzania (FCC).

Dar es Salaam. Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), imewataka washindani katika biashara kujiepusha na vitendo vinayolenga kufifisha ushindani sokoni huku ikijipanga kutoa elimu hiyo kwa makundi sita ya wadau katika uchumi.

Makundi hayo ni pamoja na wachimbaji madini wadogo, wazalishaji na wasambazaji wa mbegu na maua, wakamuaji wa mchuzi wa zabibu na mafuta ya alizeti, wafanyabishara wenye viwanda na wakulima wa zao la korosho.

FCC inatoa elimu hiyo ikiadhimisha wiki ya ushindani duniani ambayo kilele chake hufanyika kila ifikapo Desemba tano.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki hiyo jijini Dar es Salaam leo, Novemba 29, 2023, Mtendaji Mkuu wa FCC, William Erio amesema washindani hawaruhusiwi kupanga bei kwa shughuli wanazofanya.

Mbali na kupanga bei, Erio amesema pia hawaruhusiwi kukubaliana kupunguza uzalishaji, kupanga zabuni baina yao na kuingia mikataba yoyote inayolenga kufifisha ushindani sokoni.

"Kwa maneno mengine washindani hawaruhusiwi kula njama kufanya vitendo vitakavyochochea kufifisha ushindani baina yao kiasi cha kuleta athari kwa walaji kuongezewa bei au kuwapunguzia aina ya kuchagua," amesema na kuongeza:

"Hivyo tutakutana na wadau hao kwenye kanda, wito wangu naomba wote waliotaja kujitokeza kwa wingi katika maeneo tuliyoainisha, ili waweze kunufaika elimu itakayokuwa inatolewa," amesema Urio.

Amesema watakutana na wachimbaji wadogo wa madini wa Kanda ya Ziwa katika kusanyika litakalofanyika Mkoa wa Shinyanga.

"Kanda ya Kaskazini, tutakutana na wazalishaji na wasambazaji wa mbegu na maua mkoa wa Arusha, huku wakamuaji wa mchuzi wa zabibu na mafuta ya alizeti, tutakutana nao mkoani wa Dodoma. Vile vile mkoani mbeya, tutakutana na wafanyabiashara na wenye viwanda kwa Nyanda za Juu Kusini, huku wakulima wa korosho tukikutana nao Mkoa wa Mtwara," amesema Urio

"Sherehe za kilele zitafanyika katika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam Posta na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na biashara, Dk Ashatu Kijaji," amesema.

Akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa siku ya ushindani duniani, Erio amesema ni kuelimisha umma umuhimu wa kuzingatia kanuni za biashara ambazo zinasaidia biashara ifanyike kwa misingi ya haki na kuoa fursa sawa kwa wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa Bandia wa FCC, Khadija Ngasongwa amesema katika mikutano yao watawaeleza wahusika kuhusu athari za kupanga njama na namna wanavyopaswa kujiepusha na vitendo hivyo kwa masilahi ya kulinda ushindani kwa masilahi ya walaji.