Hivi ndivyo Magufuli atakavyozikwa

Hivi ndivyo Magufuli atakavyozikwa

Muktasari:

  • Ni huzuni na majonzi. Ndivyo unavyoweza kuizungumzia siku ya leo Ijumaa Machi 26, 2021 wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wa Serikali, majeshi ya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, dini na wananchi wa mkoa wa Geita katika mazishi ya hayati John Magufuli.

Chato. Ni huzuni na majonzi. Ndivyo unavyoweza kuizungumzia siku ya leo Ijumaa Machi 26, 2021 wakati Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wa Serikali, majeshi ya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, dini na wananchi wa mkoa wa Geita katika mazishi ya hayati John Magufuli.

Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo akazikwa katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato.

Kwa mujibuĀ  Sheria ya Maziko ya viongoziĀ  ya mwaka 2006 kifungu cha 20(1-4) inaeleza utaratibu siku ya mazishi ya Rais.

Kutokana na sheria hiyo, mambo manne yakiwa katika mfumo wa taratibu za kijeshi yanatazamiwa kufanyika.

Kutakuwa na gwaride maalumu litakaloandaliwa na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Wakati wa gwaride hilo litakaloandaliwa kwa heshima ya Rais anayezikwa, pia utaimbwa wimbo wa Taifa.

Pia katika shughuli hiyo, askari wa JWTZ watapiga mizinga 21 wakati wa mazishi hayo karibu na eneo linalofanyika maziko ya Rais aliyefariki.

Jambo la nne, utaratibu mzima wa ufanyikaji wa gwaride hilo unatakiwa kufuata maelekezo ya Waziri ambaye ana dhamana ya kusimamia masuala ya ulinzi.