Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu ya kina Mramba yaiva

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basir Mramba (kulia) aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja(kushoto) na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis.

Muktasari:

Vigogo hao watatu wameshtakiwa kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi

Dar es Salaam. Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa hukumu katika kesi inayowakabili mawaziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na wa Nishati na Madini, Daniel Yona pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Monja, Juni 30, mwaka huu.

Kesi hiyo inasilikilizwa na jopo la mahakimu watatu, John Utamwa, Sam Rumanyika na Saul Kinemela. Viongozi hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mashahidi saba wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi na kuwasilisha vielelezo vyao vilivyopitiwa na mahakama na kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu hivyo kuwataka watoe utetezi wao dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

Katika maandalizi ya kuwasilisha hoja za kushawishi mahakama iwaone washtakiwa hao wana hatia ama la, Jumatatu ijayo mahakama itazipatia pande hizo mbili mwenendo wa kesi nakala ya mwenendo wa kesi ili waweze kuandaa hoja zao za kuishawishi na kuziwasilisha mahakamani.

Kwa mujibu wa kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2008, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

Katika utetezi wa Mgonja, alidai kuwa yeye ndiye aliyemshauri Waziri Mramba kuisamehe kodi kampuni hiyo iliyokuwa ikifanya kazi ya kukagua madini ya dhahabu nchini, kwa sababu kulikuwa na mkataba uliosainiwa Juni, 2003 kati ya kampuni hiyo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) uliokuwa unaonyesha malipo yafanyike bila ya kukatwa kodi.