Huyu ndiye pacha aliyeteuliwa kuwa Jaji

Huyu ndiye pacha aliyeteuliwa kuwa Jaji

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji 28 wa Mahakama Kuu Tanzania ambapo, miongoni mwao ni Dk Eliamani Isaya Laltaika.

Arusha. Ni vigumu sana kuwatofautisha mapacha mawili ambao wote ni madaktari wa Sheria na sasa mmoja ameteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Madaktari hawa bingwa wa sheria wamezaliwa Kijiji cha Nainokanoka wilayani Ngorongoro, ambapo Dk Eliamani Isaya Laltaika ndiye ameteuliwa kuwa Jaji. Kabla ya wadhifa huo mpya alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Tumaini Kampasi ya Dar es Salaam (Tudarco).

Pacha wake Dk. Elifuraha Isaya Laltaika yeye anaendelea na majukumu yake akiwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira jijini Arusha.

Katika mahojiano yake na Mwananchi, Dk Elifuraha amesema watu wengi wamekuwa wakiwachanganya hivyo kuwa wachangamoto kubwa.

"Kuna changamoto, watu wengi wamekuwa wakituchanganya sana na inakuwa kazi ngumu kututofautisha. Hata baada ya uteuzi, wengi wamenipigia simu kunipongeza wakati ndugu yangu ndio ameteuliwa kuwa Jaji,” amesema Dk Elifuraha ambaye ndiye mdogo.

Kwa upande wake, Dk Eliamani amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Jaji na kwamba, ataifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa.

Kwa undani zaidi kuhusu mapacha hawa na mambo mbalimbali ikiwemo maisha na familia zao, usikose kusoma gazeti la Mwananchi  Ijumaa ya Mei 14, 2021.