Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Idadi ya vifo Hanang yafika 85

Sehemu ya nyumba za makazi ya Wananchi wa eneo la Jorodom, Katesh Wilayani Hanang likiwa tupu mara baada ya kupitiwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe hali iliyopelekea uharibifu unaonekana pichani.

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa jana hadi saa sita mchana vifo vilikuwa 80, ila taarifa iliyotolewa leo na Serikali imeeleza kuwa idadi ya vifo hivyo imeongezeka na kufikia 86.

Hanang. Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya matope, mawe makubwa na magogo ya miti kutoka mlima Hanang imeongezeka na kufikia 85.

Kwa mujibu wa  taarifa ya Serikali ya hali ya maafa yaliyotokea wilayani Hanang, iliyotolewa leo Desemba 9,2023 na Msemaji Mkuu wa  Serikali, Mobhare Matinyi imesema miili yote 85 imeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa.

Kuhusu idadi ya majeruhi amesema waliopokelewa katika hospitali za mkoani Manyara ilifikia 139 ila waliopo hospitalini ni 51.

"Jumla ya majeruhi 86 wamepata nafuu na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku wawili wakifariki. Kutokana na juhudi za Serikali za kuwapa ushauri nasaha, kuwasaidia kupata mahitaji muhimu na chakula pamoja na kuwaunganisha na ndugu na jamaa zao waathirika kwenye kambi wamepungua kutoka 440 hadi 322,"ilisema taarifa hiyo

Taarifa hiyo imesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za maji ili kulinda afya za wananchi katika kipindi hiki ambapo imeleta matanki ya lita 5,000 na kuyagawa katika mitaa na vijiji kadhaa, huku ikisambaza maji kwa kutumia malori kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo popote walipo.

"Serikali pia imeendelea kutoa elimu ya afya kwa umma na vilevile imesambaza dawa za kutibu maji kwenye kaya 1,300 katika eneo la waathirika ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, na kuzuia magonjwa ya kuhara,"imesema taarifa hiyo.