IEBC yasalimu amri

Saturday August 06 2022
uchaguzi pic

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati

By Mwandishi Wetu

Nairobi. Hatimaye Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini Kenya, imesema itatekeleza amri ya mahakama ya kuweka daftari la wapiga kura walioandikishwa kieletroniki kwa ajili ya uhakiki kabla ya upigaji wa kura kufanyika.

Juzi Mahakama iliridhia shauri lililofunguliwa na mgombea urais wa Azimio la Umoja, Raila Odinga aliyetaka kutumika kwa daftari la wapiga kura kuhakiki majina ya wapiga kura badala ya kutumia mfumo wa kieletroniki pekee kama walivyotaka IEBC.

Jana Ijumaa Agosti 5, 2022 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amethibitisha utekelezaji wa amri hiyo.
Ikiwemo kuridhia uhakiki wa kawaida  kwenye kuandikisha na kuhakiki wapiga kura.
Chebukati amesema kuwa nakala zilizochapishwa za majina ya wapiga kura zitapatikana nchi nzima kwa ajili ya kuhakiki uandikishwaji wa kielektroniki uliofanyika awali.
Tume pia imesema kuwa pallet 4,433 zimewasili nchini humo na kundi la mwisho la pallet 18 zinatarajiwa kuingisha kesho. Chebukati amesema kuwa vifaa vyote vinavyohusiana na uchaguzi vitasambazwa nchi nzima hadi kufikia jumapili hii.

Advertisement