Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jela miaka 30 kwa kumlawiti mwanafunzi Katavi

File Photo

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Katavi jana Agosti 9,2023 imewahukumu kutumikia miaka 30 jela, Majid Khalid almaruufu Alsalimi (36)  mkazi wa Mtaa wa  Madukani, na Wahab Amory (29) mkazi wa Mtaa wa Kawajense, Manispaa ya Mpanda; baada ya kupatikana na kosa la kulawiti.

Katavi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Katavi jana Agosti 9,2023 imewahukumu kutumikia miaka 30 jela, Majid Khalid almaruufu Alsalimi (36)  mkazi wa Mtaa wa  Madukani, na Wahab Amory (29) mkazi wa Mtaa wa Kawajense, Manispaa ya Mpanda; baada ya kupatikana na kosa la kulawiti.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Katavi, Gway Sumaye, ambapo mbali na adhabu hiyo, wawili hao wanatakiwa kumlipa muathirika wa tukio hilo Sh2 milioni kila mmoja ikiwa ni fidia.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, watu hao walitenda kosa hilo la kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kwa nyakati tofauti, jambo ambalo ni kinyume na kifungu namba 154(1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16.

Watu hao wanadaiwa kutenda kosa hilo maeneo ya madukani, Shanwe na Kawajense Manispaa ya Mpanda kwa nyakati tofauti kuanzia March 1, 2022 hadi March 2023.

Taarifa za kimahakama zinaonyesha kuwa kesi ilifunguliwa na kuanza kusikilizwa mahakamani hapo   April 24, 2023.