Jeshi la Polisi Mufindi lapokea msaada

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa limepokea msaada wa tenki la maji lenye ukubwa wa lita 5000 kwa Kampuni ya Kapondogoro Auction Mart  huku  thamani yake ikiwa zaidi ya Sh800,000

Mufindi. Jeshi la Polisi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa limepokea msaada wa tenki la maji lenye ukubwa wa lita 5000 kwa Kampuni ya Kapondogoro Auction Mart  huku  thamani yake ikiwa zaidi ya Sh800,000

Akipokea msaada huo Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la polisi Wilaya ya Mufindi, Alfred Mbena amesema uwepo wa tenki la maji dogo ambalo lilikuwa halikidhi mahitaji hivyo kuletea Kwa tenki hilo nimsaada mkubwa kwao.

Aidha Mbena amesema kuwa licha ya kukabidhiwa kwa tenki hilo  polisi  jamii imekuwa ikishirikiana wananchi katika masuala mbalimbali ili kuweza kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

" tulikuwa tukitaka  maji lazima uweke tokeni ndipo yatoke ukizingatia hapa sisi tuna matumizi makubwa ya maji hali ambayo ilitulazimu kuchimba kisima na kununua pampu naisihi jamii wasichoke  kutusaidia  wao kama wadau wa polisi  katika kutoa misaada kama hii kwa jeshi la polisi si kwa mafinga tuu bali hata katika Maeneo mengine." Amesema Mbena

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Mafinga, Christopher Msonsa amsema tanki hilo la maji litasaidia kuhifadhi maji kwa ajili ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kunawa mikono kwa ajili ya  kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19.

"Tunaishukuru kampuni ya Kapondogoro kwa kutupatia tank la lita elfu 5000 kwa ajili ya kuifadhia maji kwa sababu hapo awali tulikuwa na tanki ndogo la lita 1000 hivyo uwepo wa tanki hil  litasaidia kupunguza adha ambayo tulikuwa tunaipata." Amsema  Msonsa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Kapondogoro Auction Mart , Methew Mkumbo amesema kuwa kampuni hiyo iliamua kutoa msaada huo wa  tenki la maji kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina yao na jeshi hilo.