Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiji la Dodoma latoa mikopo ya Sh3.4 bilioni

Muktasari:

  • Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa Sh3.4 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa vikundi 340 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.



Dodoma. Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa Sh3.4 bilioni katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa vikundi 340 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Hayo yamesemwa leo Juni 25,2022 na Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri hiyo, Sigilinda Mdemu kwa niaba ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Joseph Mafuru wakati wa kukabidhi hundi za mfano.

Amesema Sh1.58 bilioni ilitolewa kwa vikundi 124 vya wanawake, Sh 1.67 bilioni kwa vikundi vya vijana na Sh170.6 bilioni kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.

“Utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia Juni 2022, ulitolewa kwa awamu nne kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu,”amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amesema kuwa katika mwaka 2022/2023, wametenga Sh1.3 bilioni kwa ajili ya kujenga kituo cha ujasiriamali kwenye eneo la Nzuguni ambalo litatumika katika uchakataji wa bidhaa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amesema changamoto kubwa ni maeneo ya kufanyia ujasiriamali kwa vikundi ambapo vingi vimekuwa vikifanyia majumbani.

“Ofisa Maendeleo Jamii kaa na vikundi vyote unihodhoresheni vikundi ambavyo havina maeneo ya kufanyia shughuli, ili tukaa nao, tunaweza kupata makubaliano ya mikataba ya muda mrefu,”amesema