Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKCI kutoa mafunzo kuhudumia wagonjwa wa dharura

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI (mwenye suti) akiwa anaingalia timu ya watalaamu waliopo kwenye mafunzo ya utoaji huduma za dharura na mahututi katika Hospitali ya Dar Group leo mkoani Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Serikali kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imewapa mafunzo madaktari watakaowahudumia wagonjwa wa dharura na wale mahututi katika kitengo cha huduma za dharura hospitali ya Dar group pamoja na ununuzi wa vifaa tiba, sambamba na upimaji wa maradhi bure.

Dar es Salaam. Katika kuboresha huduma kwa wagonjwa mahututi na wale wa dharura, Serikali kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imewapa mafunzo madaktari watakaotoa huduma hiyo, ununuzi wa vifaa tiba, sambamba na upimaji wa maradhi bure.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 31, 2023 alipokuwa katika Hospitali ya Dar Group iliyopo Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema hatua hiyo inakuja baada ya kununuliwa vifaa vya Sh760 milioni vitakavyotumika kufanyia huduma hiyo.

Dk Kisenge amesema vifaa hivyo vinavyojumuisha mashine za upimaji moyo na wagonjwa waliozidiwa ambavyo vimefungwa katika hospitali hiyo iliyochini ya JKCI.

Amesema wananchi wa Dar hususani waliopo Wilaya ya Temeke watapata huduma hiyo ambayo awali haikuwa inapatikana hospitalini hapo. Amesema jambo hilo litapunguza mizunguko kwa wananchi. 

“Tumetoa elimu kwa madaktari na manesi jinsi ya kuwahudumia wagonjwa hao na mafunzo haya yatakuwa endelevu kwa madaktari hao,” amesema Dk Kisenge.

Aidha, amesema wataendesha zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali bure ikiwemo yale ya moyo hospitalini hapo kwa siku mbili kuanzia Septemba 2 na 3.

“Nitoe wito kwa wakazi wa Dar, wajitokeze waje wapime magonjwa ili kutambua afya zao. Wakifanya hivyo wataiepushia Serikali gharama ambazo ingetumia kuwatibu watu,” amesema Dk Kisenge.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa upasuaji na Msimamizi wa Kitengo cha Magonjwa ya dharura na wagonjwa mahututi, Dk Angela Muhozya, amesema wanapokea wagonjwa wote wa dharura na mahututi kisha watampatia ruhusa ya kwenda hosptitali ya ngazi ya kitaifa ikiwa inahitajika.