Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jubilee yashinda tuzo ya huduma bora

Dereck Rwezaura na Gift Swai kutoka Jubilee Life Insurance katika hafla  ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na Charted Instute of Customer Management, ambapo kampuni hiyo imeibuka mshindi katika utoaji huduma bora kipengele cha bima.

Muktasari:

  • Kampuni ya Jubilee Insurance Corporation Tanzania Limited imeibuka mshindi kati ya kampuni bora za utoaji huduma za bima ya maisha.

Dar es Salaam. Kampuni ya Bima ya Jubilee Life Insurance, imeshinda tuzo ya utoaji wa huduma bora katika kipengele cha bima za maisha kwa wateja.

 Tuzo hizo zinazotolewa na taasisi ya Chartered Institute of Customer, vigezo vya ushindi ni kuangalia utoaji huduma wa kampuni mbalimbali kwa wateja.

Kwa maneno mengine, ushindi huo kwa Jubilee unamaanisha ndiyo kampuni bora kwa utoaji wa huduma za bima za maisha kwa wateja wake.

Akizungumza katika hafla ya utolewa wa tuzo hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jubilee Insurance, Helena Mzema amesema hiyo ni ishara ya heshima kwa kampuni hiyo.

Amesema hatua hiyo inaongeza hamasa kwa kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma bora za bima kwa wananchi.

“Hii inaendelea kutupa hamasa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi, mwaka jana ulikuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa na sasa tumejipanga ipasavyo kuwahudumia wateja wetu kwa viwango vya juu,” amesema.

Ameeleza kwa sasa huduma ya bima ya maisha kutoka kampuni hiyo imejikita kidigitali, ili kurahisisha upatikanaji wake.

 “Tunawashukuru sana wateja wetu na wale wote walioshiriki kwenye mchakato wa kupata mshindi wa tuzo ya huduma bora na inaendelea kutoa bima bora za Maisha zinazolinda ndoto za wateja wetu na wapendwa wao,” amesema.