Kampuni zaongeza nguvu huduma za bima

Tuesday May 17 2022
BIMA PIC
By Ephrahim Bahemu

Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea na mkakati wake wa kuongeza ushiriki wa ananchi katika huduma za bima kampuni huduma za simu ya Vodacom kwa kushirikiana na Milvik, Jubilee Insurance na Mo Assurance wameanzisha huduma ambayo itajumuisha watu wengi zaidi.

Serikali imepanga hadi kufikia mwaka 2030 elimu ya bima iwe imewafikia wananchi kwa asilimia 80 na asilimia 50 ya wananchi wawe wanatumia huduma za bima tofauti na sasa ambapo watumiaji wa huduma za bima ni asilimia 15 to ya wananchi wote.

Kupitia ushirika huo kampuni hizo zimeanzisha huduma za bima kwa ajili ya matibabu, ajali na maisha kwa kiasi kidogo cha Sh4, 000 kwa mwezi kwa mtu mmoja na kila mwanafamilia anayeongezeka atalipiwa Sh750 kwa mwezi hadi wanafamilia watano.

Akishuhudia uzinduzi wa huduma hizo juzi Mei 15, Meneja Utekelezaji Sheria na kushughulikia malalamiko katika Mamlaka ya bima nchini (TIRA), Okoka Mgavilenzi amesema kutokana na unafuu wa huduma hiyo matarajio ya kuongezeka kwa watumiaji wa huduma za bima nchini ni makubwa hivyo alipongeza kwa ubunifu wa makampuni hayo.

“Watu wa kipato cha chini wamekuwa hawapat huduma kama hizi za bima ya afy hivyo wanapougua wanakuwa hamana uhakika wa gharama za kujihudumia lakini sasa lakini hii itawasaidia,” alisema Mgavilenzi huku akitoa msisitizo kwa watoa huduma kuhakikisha madai yanashughulikiwa kwa wakati pindi yanapowasilishwa.

Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni amesema huduma ya bima ya afya ni huduma muhimu kwa watu wote lakini sio watu wote wanaweza kumudu gharama zake ndiyo maana Vodacom na washirika wao wakaja na huduma hiyo ambayo itawalenga zaidi watu wenye kipato cha chini ambao awali aikuwa rahisi kwao kupata huduma za hizo.

Advertisement

 “Tuna furaha kubwa leo kuweza kutangaza maendeleo haya muhimu katika utoaji wa bima kwa Watanzania. Vodacom Tanzania imeweka mkazo mkubwa kwenye afya kama kichocheo kikuu cha shughuli zetu zinazoongozwa na malengo. Huduma ya afya ni hitaji la msingi kwa Watanzania wote na tunaamini inapaswa kupatikana kwa urahisi kwa wote,” amesema Mbeteni.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Milvik, Ismail Simanga amesema huduma hiyo ni hatua kubwa inayotoa uhakika wa kulinfda afya ya familia znye kipato tofauti hususani kidogo na kizuri zaidi ni kuwa huduma hizo zinapatikana kwa njia ya simu.

“Afya na usalama wa famila ni kila kitu kwa kila mtu, unataka kukusaidia kuwalinda wapendwa wako dhidi ya hali zilizo nje ya uwezo wako bina hii ni suluhisho, mafao kwa aliyejiunga ukilizwa ni sh30,000 kila siku, kupoteza maisha ni Sh3milioni na ulemavu wa kudumu ni Sh3milioni,” amesema Simanga.

Advertisement