Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jumuiya ya Ismailia yaiunga mkono Serikali

Muktasari:

  • Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 58,000 wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Ismaili duniani kote, kati ya Septemba na Oktoba 2023; wameshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kuadhimisha Siku ya tatu ya Kimataifa ya Ismailia ya CIVIC.

Dar es Salaam. Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 58,000 wa Jumuiya ya Waislamu wa Shia Ismaili duniani kote, kati ya Septemba na Oktoba 2023; wameshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kuadhimisha Siku ya tatu ya Kimataifa ya Ismailia ya CIVIC.

Shughuli hizo ni pamoja na upandaji wa miti, uokotaji wa taka pamoja na uchangiaji wa damu kwa wenye uhitaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Mawasiliano Ismaili CIVIC, Aliza Hasham inaeleza kuwa shughuli hizo zilihusisha nchi 30, ikiwa ni pamoja na Tanzania, na kushirikiana na washirika mbalimbali kama vile Aga Khan Foundation (AKF), World Wildlife Fund (WWF), Prince’s Trust, City of Houston, Natural History Museum (UK), Emirates Marine Environmental Group, American Red Cross, Indian Red Cross, Green Savers, na River Clean-up.

“Kupitia Ismaili CIVIC, jumuiya ya Ismailia duniani kote inaendeleza utamaduni wake wa karne nyingi wa kutoa huduma ya hiari ili kuboresha maisha ya jamii wanamoishi, bila kujali imani, jinsia na asili,” inaeleza.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa nchini Tanzania, zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea 200 walikusanyika pamoja na wafanyakazi wa AKF kwa ajili ya "Go Green Festival" ambayo huadhimishwa kila mwaka wakati wa Siku ya Kimataifa ya Ismaili CIVIC.

Kupitia mradi huo wa Go Green wameweza kukuza msitu mdogo wa Upanga Jamatkhana kwa kupanda zaidi ya miche 200 na kuongeza miche 100 baada ya kuanzishwa kwa shamba hilo mnamo Februari 2023 pamoja na kujifunza jinsi ya kulima mboga zao wenyewe na kuzalisha kupitia warsha ya bustani ya nyumbani.

Vile vile, wanajamii wa Morogoro, Dodoma, Mwanza na Tabora wamejitolea kupanda miche 1,100 ya mikoko ili kusaidia juhudi zinazoendelea za uondoaji kaboni.

“Tangu kuzinduliwa kwake kimataifa mnamo 2021, Siku ya Kimataifa ya Ismaili CIVIC imekuwa na athari kubwa katika afya, elimu, maendeleo ya kiuchumi na utunzaji wa mazingira. Wakishirikiana na mashirika zaidi ya 600, wafanyakazi wa kujitolea kutoka nchi 33, ikiwa ni pamoja na Tanzania wamechangia zaidi ya saa 455,000 za huduma”inaeleza

Tangu kuzinduliwa kwake kimataifa mnamo 2021, Siku ya Kimataifa ya Ismaili CIVIC imekuwa na athari chanya na kubwa katika afya, elimu, maendeleo ya kiuchumi na utunzaji wa mazingira.

Ulimwenguni kote, kupitia mpango huu, zaidi ya miti milioni tatu imepandwa, takriban kilo 163,000 za taka zimeondolewa kutoka katika mbuga, mito, fukwe na mijini, na zaidi ya chupa za damu zimepatikana kusaidia watu wenye uhitaji.

Kuhusu Jamii ya Waismailia

 Jumuiya ya Ismailia kama sehemu ya dhehebu la Shia katika dini ya uislamu ni watu wenye tofauti za lugha na mila mbalimbali wakiishi katika nchi zaidi ya 25 duniani.

Jumuiya hii inaendeleza na kutukuza jadi ya ki-Shia ya miaka 1,400 ya kuenzi utafutaji wa maarifa kwa nia kujiendeleza binafsi na jamii; kuheshimu tofauti baina ya watu, kuendeleza na kulinda amani na maelewano kuchangia muda wao, rasilimali walizo nazo na ujuzi wao ili kuboresha maisha ya watu na jamii zao