Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JWTZ kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Muktasari:

  • Moto huo ulioanza kuwaka Oktoba 21, 2022 katika eneo la Karanga lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka.

Dar er Salaam. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa baadhi ya maofisa na askari wake wamewasili kuanza operesheni ya kuzima moto unaoendelea kuwaka katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

 Moto huo ulioanza kuwaka Oktoba 21, 2022 katika eneo la Karanga lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka, bado haujadhibitiwa.

Oktoba 23 mwaka huu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Eliamani Sedoyeka alisema kuwa Serikali imeliomba Jeshi la Wananchi (JWTZ) kuongeza nguvu ili kuweza kuudhibiti moto huo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo leo Jumanne Novemba 1, 2022 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi hilo, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda imesema kuwa “Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ameamuru JWTZ kushiriki operesheni ya kuzima moto huo unaoendelea kusambaa.

Maofisa na Askari wa JWTZ tayari wamewasili maeneo ya Siha na Mwika Mkoani Kilimanjaro tayari kuanza Operesheni ya uzimaji wa moto huo” imesema taarifa hiyo.

“JWTZ litashirikiana kikamilifu na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama,wadau mbalimbali na wananchi ili kuhakikisha moto huo unadhibitiwa mapema kabla ya kuleta madhara makubwa katika Hifadhi hiyo. Aidha, JWTZ litaendelea kusaidia Mamlaka za kiraia pale litakapohitajika” imesema taarifa hiyo.