Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kampuni za ndani nje zaongoza kupewa kazi za uhandishi nchini

Mwenyekiti wa ERB, Wakili Menye Manga

Muktasari:

  • Wahandisi wa Tanzania wamesema wamekuwa na ushiriki mdogo kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Licha ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati, Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), imesema bado zinazoaminiwa kupewa kazi hizo ni kampuni za kihandisi za nje ya Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Septemba 14, 2023 na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Wakili Menye Manga katika hafla ya maadhimisho ya 20 ya siku ya Wahandisi nchini.

Amesema ushiriki wa wahandisi wa Tanzania pamoja na kampuni zao katika miradi nchini ni mdogo.

Kinachoshangaza, amesema baadhi ya miradi zinapaswa kampuni za nje ya nchi zenye mazingira yanayofanana na Tanzania.

Lakini, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuongeza ufanisi wa wahandisi nchini ili waendelee kuaminiwa na kutumiwa katika miradi nchini.

"Mikakati ya kufikia shabaha hiyo ni kuongeza ujuzi wa kitaaluma na tunaendelea kufanya hivyo," amesema.

Kuhusu mkutano huo, amesema matarajio ni kutoka na maazimio yatakayowasilishwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

"Tutakuwa na mabadiliko katika sheria na kanuni zetu ili kuongeza usajili zaidi wa wahandisi," amesema.

Lakini, katika hafla hiyo, amesema wahandisi 200 wataapa kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na kuzingatia maadili ya kazi ya uhandisi.

"Kiapo watakachokula leo ni cha maisha anaapa kutekeleza majukumu yake ya kihandisi kwa maadili miaka yote," amesema.

Hata hivyo, amesema vyuo vya Tanzania kwa sasa vinazalisha wahandisi 3,500 wanaoingia katika soko la ajira kila mwaka na kwamba mpango wa mafunzo tarajali utaandaliwa kwa ajili ya kuwaendeleza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wakati anasoma wazazi wake walimlazimisha kusomea sayansi kwa ajili ya taaluma hiyo.

Amesema kipindi hicho ni wahandisi wachache waliokuwa wakipata kazi, akisema ndiyo sababu hata George Simbachawene (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu) kuachana na taaluma hiyo na baadaye kusomea sheria.

Lakini, amesema kwa sasa kuna mabadiliko na maeneo makubwa.

"Ukiiangalia taaluma hii kwenye vitabu miaka ya nyuma, tujue kwamba kuna wajibu mnapaswa mtimize kubadili uchumi wa nchi ili isonge mbele," amesema.