Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KESI YA MAUAJI: Daktari aeleza mtoto Masumbuko alivyofariki kwa kukosa hewa

Zephania Ndalawa anayeshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Thomas Masumbuko akiwa Mahakamani muda mfupi kabla ya kesi kuanza. Picha na Rehema Matowo

Muktasari:

  • Uchunguzi wa kitabibu uliofanywa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Senga Wilaya ya Geita ulibaini mtoto Thomas Masumbuko (12) alipoteza maisha kwa kukosa hewa baada ya kuingiziwa matambara mdomoni na puani.

Geita. Shahidi wa sita katika shauri la mauaji linalomkabili Zephania Ndalawa, anayeshtakiwa kwa kumuua kwa kukusudia Thomas Masumbuko, ameieleza Mahakama namna alivyokuta mwili wa marehemu ukiwa na kinyesi na mkojo huku ulimi ukiwa umetoka nje.

Shahidi huyo, Clever Shaban ambaye ni Ofisa Tabibu katika Zahanati ya Senga iliyopo wilayani Geita, aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, ameeleza kuwa Agosti 19, 2024 akiwa kazini kwake, alipigiwa simu na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Senga akimweleza kuna tukio la uvamizi lililosababisha majeruhi na kifo.

Amedai kuwa baada ya taarifa hizo, alifika eneo la tukio na kukuta polisi pamoja na ndugu wa familia na kutambulishwa, kisha wakamwingiza kwenye chumba alichokuwa marehemu na kukuta mwili ukiwa kitandani umelala chali.

Ameeleza katika kuchunguza mwili huo, alibaini ulikuwa umetokwa na damu puani na mdomoni huku ulimi ukiwa nje na kwenye nguo kulikuwa na kinyesi na mkojo, dalili ambazo kitabibu hutokana na mtu kukosa hewa.

Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Deodatha Dotto amefafanua mtu kutokwa kinyesi na mkojo na ulimi kuwa nje, inamaanisha alikuwa akihangaika kutafuta hewa.

 “Uchunguzi niliofanya nilibaini marehemu alifariki kwa kukosa hewa. Nguo zilikuwa zimechafuka kinyesi na mkojo, ulimi umetoka nje, puani na mdomoni kulikuwa na damu na hakuwa amefunga macho na hii inaonyesha alikuwa akihangaika kutafuta hewa,” ameeleza Shaban.

Akiulizwa maswali ya dodoso na Wakili wa Utetezi, Beatrice Amos kwamba mtu aliyewekewa matambara mdomoni ulimi unakuwaje nje, shahidi huyo alieleza kuwa inawezekana kwa kuwa alikuwa akihangaika kutafuta hewa.

Pia, amehoji iwapo mgonjwa wa pumu anaweza kupoteza maisha kwa kukosa hewa? Shahidi huyo alidai inawezekana lakini yeye hakupewa historia yoyote kuwa marehemu alikuwa na tatizo la pumu.

Shahidi mwingine, Bihali Nyalema, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Senga, ameieleza Mahakama kuwa Agosti 19, 2023 akiwa kazini, alipigiwa simu na mwenyekiti wa Kitongoji cha Msilale, Balawai Misana akimweleza kuwa kwenye eneo lake kuna tukio la uvamizi.

Amedai baada ya taarifa hizo, alifunga safari hadi kwenye tukio na kumpigia mkuu wa Kituo cha Polisi Kakubiro, aliyemuahidi kufika na walipofika pamoja na daktari aliwaongoza hadi kwenye chumba alichokuwa amelazwa marehemu.

“Nilipoingia kwenye chumba alichokuwa Thomas (marehemu) alikuwa na mapovu mdomoni na ulimi ukiwa umetoka nje na kwa pembeni kulikuwa na nguo alizokuwa amefunikwa kichwani, majeruhi sikumkuta alikuwa ameshawahishwa hospitali,” ameeleza Nyalema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Julai 4, 2024 itakapoendelea hatua ya ushahidi wa mashtaka.