Kimiti astaafu bodi ya Narco akieleza mafanikio

Thursday October 14 2021
Kamti pc
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Ranchi za Taifa (Narco), Paul Kimiti amesema ndani ya miaka mitatu ya  bodi hiyo imefanikiwa  kukodisha maeneo kwa ajili ya wafugaji kufuga mifugo yao hali iliyosababisha kupunguza migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Ahamisi 14, 2021 na wizara hiyo, imeeleza kuwa   bodi hiyo imemaliza muda wake baada ya kukaa madarakani kwa miaka mitatu.

Pia imeweza kusimamia na kuhakikisha wafugaji nchini wenye mifugo mingi wanapatiwa maeneo kwa mikataba katika ranchi za Narco kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

“Tumegawa maeneo ya ranchi takribani asilimia 75 na kubakiza asilimia 25 kwa kuwa wafugaji nchini wamekuwa na mifugo mingi na wanahitaji maeneo kwa ajili ya kufuga mifugo yao,” amesema Kimiti.

Amefafanua kuwa ndani ya miaka mitatu bodi ya wakurugenzi ya Narco imehakikisha maeneo ya ranchi za taifa yanawekewa mipaka ili kuzuia uvamizi wa maeneo hayo,akisema mchakato huo unaendelea katika  maeneo mengine yasiyowekewa alama hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Narco, Profesa Peter Msoffe, amesema bodi ya wakurugenzi iliyomaliza muda wake imeweka misingi sahihi katika kufuatilia ukubwa wa maeneo ya ranchi, madeni na mashauri mbalimbali yaliyoiwezesha kwa kiasi kikubwa yameiwezesha kupata mafanikio zaidi.

Advertisement

Amesema bodi hiyo imekuwa ikitoa maelekezo kwa Narco ya  kuhakikisha inakaa na wawekezaji waliopatiwa  wamepatiwa vitalu katika ranchi za kampuni hizo  kuona namna ya kuboresha mikataba ili kuzinufaisha pande zote mbili.

Advertisement