Kinachofuata baada ya Ndugai kujiuzulu

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Muktasari:

Kwa mujibu wa tangazo la katibu huyo wa Bunge liliyotolewa leo Ijumaa Januari 7, 2022 kwa wabunge, amesema hakuna shughuli zitakazoendelea kwa kipindi ambacho nafasi ya Spika iko wazi hivyo amewaagiza wabunge wote kufika Dodoma Januari 31, 2022 kwa ajili ya kuanza Mkutano we Sita we Bunge utakaoanza Februari Mosi.

Dar es Salaam. Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi ya Spika zinaendelea huku akitangaza kuahirishwa vikao vya Kamati za Bunge ambavyo vilipangwa kuanza wiki ijayo.

 Kwa mujibu wa tangazo la katibu huyo wa Bunge liliyotolewa leo Ijumaa Januari 7, 2022 kwa wabunge, amesema hakuna shughuli zitakazoendelea kwa kipindi ambacho nafasi ya Spika iko wazi hivyo amewaagiza wabunge wote kufika Dodoma Januari 31, 2022 kwa ajili ya kuanza Mkutano we Sita we Bunge utakaoanza Februari Mosi.

Jana Alhamisi Januari 6, 2022 aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai alijiuzulu nafasi hiyo.

Katika taarifa yake kwa umma, Ndugai alisema “Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania na nakala yangu ya kujiuzulu nimeiwasilisha kwa Karibu wa Bunge” ilisema taarifa ya Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa

Muda mfupi baada ya taarifa ya Ndugai, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alithibitisha kupokea barua ya Ndugai ikimtaarifu kujiuzulu nafasi hiyo huku akibainisha kuwa utaratibu wa chama unaendelea wa kumpata Spika mwingine.

Chongolo alisema “Baada ya kuipokea barua hiyo jukumu langu ni kumjulisha Katibu wa Bunge kuhusu uwepo wa nafasi wazi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, zoezi ambalo linaendelea kwa utarajibu wa chama na baada ya hapo mchakato wa kumpata Spika mwingine utaendelea” alisema mtendaji mkuu huyo wa CCM.

Leo, katika tangazo lake kwa wabunge Katibu wa Bunge amesema “Waheshimiwa Wabunge, kama mnavyofahamu siku ya Alhamisi, tarehe 06 Januari, 2022 Mhe. Job Y. Ndugai, Mb. alijiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taratibu za uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo zinaendelea

“Kwa mujibu wa lbara ya 84 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Spika ndiye Kiongozi wa Bunge na ndiye msimamizi wa shughuli zote za Bunge. Aidha, lbara ya 84 (8) inaelekeza kwamba Kiti che Spika kinapokuwa wazi hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge isipokuwa uchaguzi we Spika.” Amesema Katibu wa Bunge nakuongeza

“Hivyo, Kamati zilizokuwa zikutane kuanzia tarehe 10 Januari, 2022 na zilizotakiwa kukutana kuanzia tarehe 17 Januari, 2022 sasa hazitakutana kwa wakati huo na badala yake zitakutana wakati wa Mkutano we Sita we Bunge (1 — 11 Februari, 2022) kwa utaratibu na tarehe zitakazotangazwa.

“Kwa msingi huo, mnaombwa kufika Dodoma Siku ya Jumatatu tarehe 31 Januari, 2022” amesema