Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kortini akituhumiwa kutoweka na fedha za suti

Muktasari:

  • Goodluck Chang'a amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Kariakoo akituhumiwa kutoweka na fedha za suti nne zenye thamani ya Sh2.6 milioni.

Dar es Salaam. Goodluck Chang'a (42) amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kujipatia zaidi ya Sh2.6 milioni, kwa lengo la kumshonea suti nne za kiume Godfrey Jacob, matokeo yake alitoweka na fedha hizo.

Akisoma hati ya mashtaka Karani wa mahakama mbiyo, Linda Kivaju, mbele ya Hakimu, Gladness Njau alidai kuwa Julai 25, 2022 hadi Agosti 16, 2022 eneo la Posta jijini Dar es Salaam, mdaiwa alijipatia Sh1, 260, 000 kutoka kwa mlalamikaji Jacob.

Kivaju alidai kuwa mshtakiwa huyo alijipatia fedha hizo kwa lengo la kumshomea suti nne za kiume, kitu ambacho ambalo hakufanya na badala yake alitoweka na fedha hizo, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Baada ya kusomewa shtaka linalomkabili mshtakiwa huyo alikana kosa hilo.

Ndipo Jacob (mlalamikaji) aliieleza mahakama hiyo kuwa atakuwa na kielezo kimoja na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 2, 2023 kwa ajili ya kusikilizwa.