Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mume, mke kortini kwa kukutwa na meno 413 ya tembo

Washtakiwa Abdul Abdallah (wa pili kutoka nyuma) pamoja na mkewe Salama Mshamu (wa mbele) wakitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Pamela Chilongola

Muktasari:

Wanandoa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kukutwa na meno 413 ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh4.04 bilioni pamoja na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya zaidi ya Sh3.4 milioni.

Dar es Salaam. Mkazi wa Chamanzi, Abdul Abdallah (35) pamoja na mkewe, Salma Mshamu (21) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kukutwa na meno 413 ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh4.04 bilioni na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya Sh3.4 milioni.

Wanandoa hao wamefikishwa leo Julai 19, 2022 katika Mahakama hiyo wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 46 ya mwaka 2022.

Akisoma hati ya mashtaka wakili Mwandamizi Timotheo Mmari amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ambapo moja la kujihusisha na biashara ya nyara za Serikali na mawili ya kukutwa na nyara za Serikali.

Mmari alidai Januari Mosi, 2017 hadi Septemba 3, 2019 maeneo ya Saku Chamanzi wilaya ya Temeke wote kwa pamoja walinunua na kupokea meno 413 ya tembo yenye thamani ya Dola za kimarekani 1755,000 Sawa na Sh 4,040,010,000 pamoja na meno mawili ya mnyama kiboko yenye thamani ya Dola za kimarekani 1500 Sawa na Sh3,453,000.

Amedai kuwa katika shtaka la pili tarehe hiyohiyo wote kwa pamoja maeneo ya Saku Chamanzi wilaya ya Temeke walikutwa na meno 413 ya tembo yenye thamani ya zaidi ya Sh4.04 bilioni mali ya Serikali ya Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.

Mmari alidai katika shtaka la mwisho tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa wote kwa pamoja walikutwa na meno mawili ya kiboko yenye thamani ya zaidi ya Sh3.4 milioni mali ya Tanzania bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.

Amesema kuwa upelelezi wa shtaka hilo umekamilika na wanasubiri kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) aweze kuridhia kama shauri hilo liendelee mahakamani hapo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo kwa kuwa ni la uhujumu uchumi na baada ya uchunguzi kukamilika litapelekwa katika Mahakama ya Mafisadi.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 2, 2022 kwa ajili ya kutajwa