Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbilamoto awataka vijana kujiajiri kupitia teknolojia

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto akikagua simu mpya zilizozinduliwa na kampuni ya Tecno na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Dar es Salaam. Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto ametoa rai kwa vijana kujiajiri kupitia teknolojia sambamba na matumizi mazuri ya simu janja kwa ajili ya kujiingizia kipato chao.

Kumbilamoto ameyasema hayo leo Jumamosi Mei 20, 2023 katika uzinduzi wa simu janja aina ya Tecno Camon 20 Premier uliofanyika jijini hapa.

”Kampuni hii licha ya kuturahisishia mawasiliano bado inatoa fursa kwa vijana kujiajiri, maana kwa sasa fursa nyingi ziko mitandaoni. Vijana changamkieni fursa hizi na muwe na matumizi mazuri ya simu hizi,”amesema.

Kauli ya Kumbilamoto inaungwa mkono na takwimu za matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinazoonyesha idadi ya vijana nchini imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2012 hivyo wana nafasi kubwa katika kukuza uchumi na kuchangia nguvu kazi ya Taifa.

“Kulingana na tafsiri ya kimataifa, vijana ni watu wote wenye umri wa miaka 15 hadi 24. Matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa, vijana ni asilimia 19.2 ikilinganishwa na aslimia 19.1 ya Mwaka 2012,”ripoti hiyo inaonyesha.

Jasmini Mohamed, mkazi wa jijini hapa miongoni mwa wahudhuriaji wa hafla hiyo amesema teknolojia iliyotumika kutengenezea simu hiyo itamuwezesha kuongeza thamani katika biashara yake ya uuzaji bidhaa mtandaoni kwa kupiga picha zenye ubora.

“Simu hii ina kamera kubwa sana na itatusaidia sisi wafanyabiashara za mtandaoni kwasababu ukubwa kamera yake yenye Megapixel 108+50+2, nina imani wateja wangu wataziona bidhaa vizuri,”amesema Jasmini.