Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kunambi, Tarura wamaliza utata ‘Daraja la Sh31 milioni’

Muktasari:

Baada ya kuibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gharama ya ujenzi wa daraja la Mto Mngeta lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Mbunge wa Jimbo la Mlimba na Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tarura wamaeibuka na kutolea ufafanuzi.

Morogoro. Baada ya kuibuka mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu gharama ya ujenzi wa daraja la Mto Mngeta lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, Mbunge wa Jimbo la Mlimba na Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tarura wamaeibuka na kutolea ufafanuzi.


Daraja hilo limeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha ya mbunge wa Jimbo la Mlimba akiwa na baadhi ya watu wakionekana kwenye daraja hilo huku picha zikiwa na maelezo kuwa daraja limetumia Sh31 milioni.


Picha hizo zinayonyesha daraja hilo ni la mbao huku nguzo zake zikiwa za magogo.


Daraja Mngeta linaunganisha Kijiji cha Isago na Itongowa vyote vilivyopo katika Kata ya Mngeta ambapo kabla ya daraja hilo wananchi walikuwa wakivuka kwa kutumia mtumbwi.


Katika mitandao ya kijamii wengi wanajadili gharama zilizotajwa wakidai haziendani na muonekano wa daraja hilo.


Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital, Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi amefafanua kuwa daraja hilo lina urefu wa mita 40 kina cha mto ni mita 4, upana ni mita 5 na gharama za daraja ni Sh27,502,500.


Amesema gharama ya Barabara kuingia na kutoka kwenye darajani ni Sh 4, 128, 000 ambazo zinafikisha jumla ya Sh31, 630,000.


"Urefu wa nguzo ni mita 7 na unene wake ni mita 0.5, mbao ni inchi 3 kwa 8, na inchi 3 kwa 10 na aina ya mti ambao mbao zake na magogo zimetumika ni za mti aina ya Mkarati.
Aidha amesema daraja hilo litakua na uwezo wa kupitisha mizigo yenye uzito wa tani 10.


Mbunge Kunambi amesema daraja hilo litaokoa uhai wa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto ya kivuko kwani mto huu una mamba ambao wamekua wakisababisha vifo vya wananchi kila mwaka.


Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijiini (Tarura) Wilaya ya Kilombero, Mhandisi Robert Magogo amesema gharama zilizotajwa ni sahihi huku akieleza kuwa lina uwezo wa kudumu kwa miaka 10 hadi 15.


Magogo amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani daraja ni imara na kwamba kutakuwa linaangaliwa kwa ukaribu zaidi.