Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LHRC yaanika mafanikio yake kwa mwaka 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga (kulia) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya Utekelezaji wa kazi mbalimbali za LHRC Mwaka 2023  jijini Dar es Salaam leo,(kushoto) Meneja wa Usimamizi wa Ubora wa Program na kujifunza (LHRC), Neema Sembeo. Picha na Sunday George

Muktasari:

  • LHRC  yasema asilimia 90 ya mapendekezo iliyoyatoa yalijumuishwa kwenye ripoti ya Tume ya Haki Jinai.

Dar es Salaam. Miezi 11 tangu Tume ya Haki Jinai ilipowasilisha taarifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema asilimia 90 ya mapendekezo waliyoyatoa yalijumuishwa kwenye ripoti.

Julai 15, 2023 Tume inayoongozwa na Jaji mstaafu, Mohamed Chande Othman iliwasilisha kwa Rais Samia ripoti baada ya kukamilisha kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali namna ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini.

Miongoni mwa mapandekezo ambayo LHRC iliwasilisha kwa Tume ni mabadiliko ya uundwaji wa baadhi ya taasisi ili kuimarisha mfumo wa haki jinai ndani yake.

Ilipendekeza msingi wa uundwaji wa taasisi uwe kikatiba badala ya sheria ambayo muda wowote hubadilishwa.

Miongoni wa taasisi hizo ni ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Mapendekezo mengine ni kuundwa kwa chombo huru kitakachosimamia utendaji wa polisi na kutenganishwa majukumu ya taasisi au mamlaka zinazohusika na haki jinai ili kila moja itekeleze wajibu wake.

Akizungumza leo Alhamisi Juni 13, 2024 wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utekelezaji mwaka 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema kituo kinajivunia mafanikio makubwa yaliyotokana na mpango mkakati wa miaka sita kuanzia 2019 hadi 2024.

“Mapendekezo yetu ya kurekebisha mfumo wa haki jinai yalipitishwa kwa kiasi kikubwa na Tume ya Rais, asilimia 90 ya mapendekezo yetu yalijumuishwa kwenye ripoti,” amesema.

Amesema LHRC kupitia programu ya elimu kwa umma, mwaka 2023 ilifikia watu 16 milioni kupitia programu 790 za redio za kijamii.

LHRC kupitia mfumo wa Haki Kiganjani amesema ilifanyia kazi asilimia 50 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ulioripotiwa kati ya jumla ya matukio 1,919.

“Uchambuzi ulionyesha wanawake walikuwa manusura kwa asilimia 56 ukilinganisha na wanaume asilimia 44, juhudi hizi zinadhihirisha dhamira yetu ya kuboresha upatikanaji wa haki za binadamu kote nchini,” amesema.

“Masuala mengi yaliyofuatiliwa bado yanashughulikiwa katika vituo vya polisi, hasa yanayohusu jinai ambayo hayapo chini ya mamlaka ya LHRC,” amesema.

Henga amesema asilimia 12 ya masuala hayo yametatuliwa yakihusisha ngazi ya familia, polisi na Mahakama.

Amesema takribani asilimia 29 ya kesi zilielekezwa kwa msaada wa kisheria, kwa uwakilishi wa Mahakama au kuwawezesha kujitetea wenyewe hasa katika masuala yanayohusu ardhi.

Amesema wamefanikiwa kuadhimisha miaka 30 ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini, LHRC ikizindua kitabu kitakachotumika kama kumbukumbu ya historia ya mageuzi ya utetezi wa haki nchini.

“LHRC pia imefanya juhudi za kuwajengea uwezo wanawake ambao wengi wametia nia katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu katika mkoa wa Pwani.”

Amesema wanawake waliowezeshwa wanaotoka Rufiji ni 58,  Mkuranga (117), Kisarawe (100), Mafia (4), Kibaha (31), Bagamoyo (43) na Kibiti (28).