Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madaktari bingwa wa macho wahudumia 139 Newala

Daktari bingwa wa macho Amon Mwakakonyole kutoka Hospitali ya Kanda ya Kati ya Benjamini Mkapa Dodoma akimfanyia vipimo vya macho Ester Misanga Mkazi wa Newala katika kliniki maalum iliyofanyika Wilayani humo. Picha na Florence Sanawa.

Muktasari:

  • Jumla ya wagonjwa 139 wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu huku wagonjwa 35 kati yao wakifanyiwa upasuaji wa macho katika Halmashauri ya mji Newala mkoani Mtwara.

Newala. Jopo la madaktari bingwa wa macho kutoka Hospitali ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Dodoma imeweka kambi siku 8 na kufanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 35 kuwafanyia upasuaji mbambali.

 Akizungumza wakati wa kliniki maalumu ya tiba ya macho kwa wakazi wa Wilaya ya Newala, Daktari Bingwa wa Macho, Amon Mwakakonyole kutoka Hospitali ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa Dodoma alisema kuwa matatizo ya macho ni changamoto kubwa.

Alisema kuwa wengi waliofanyiwa upasuaji huo ni kutokana na changamoto ya presha ya macho pamoja na vinyama kwenye macho ambavyo vinavyosababishwa na mwanga mkali wa kuchomelea na matumizi ya kompyuta kwa muda mrefu.

“Kutokana na matatizo ya macho hata Shirika la Afya Duniani (WHO) liliwahi kushauri kuwa uchunguzi wa macho uwe unafanyika kila baada ya miaka miwili ili kuondokana na matatizo makubwa yanayoweza kusababisha kupoteza uono,” amesema.

“Magonjwa mengi ya macho yanaweza yakawa yananendelea kuaribu macho yako na wewe usione dalili yoyote mfano presha ya macho unaweza ukawa na tatizo bila wewe kujua,” amesema Dk Mwakakonyole.

Naye Mzee Sabato Mshamu ambaye ni fundi wa ushonaji nguo soko kuu Newala (mgonjwa) alisema kuwa amekuwa akiumwa macho kwa miaka mingi hivyo kushindwa kupata matibabu kutokana na hali yake.

“Serikali inafahamu hali za sisi wananchi wao ndiyo maana tunafurahi kwakutukumbuka na kutuletea matababu haya ya kibingwa nimehangaika kupata matibabu nimeenda hadi kwenye hospitali kubwa za mbali bila mafanikio kutokana na gharama kubwa hali ambayo ilinifanya nipoteze matumaini,” amesema.

Naye Salvina Clemence mkazi wa Newala (mgonjwa) alisema kuwa alipata tatizo la macho akiwa kazini na baada ya kustaafu aliendelea kuumwa macho.

“Hali ilikuwa mbaya kwa miaka zaidi ya sita sasa na leo nimepata matibabu wala sikutarajia kwa kuwa natumia Bima ya Afya nimepata matibabu sahihi pasipo kuongeza gharama yoyote,” amesema.