Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madiwani Lindi wakataa michezo kubahatisha

Muktasari:

  • Madiwani wa Manispaa ya Lindi wamesema kuwa hawataki kuona michezo ya kubahatisha kwenye manispaa hiyo, wakidai kuwa michezo hiyo inasababisha watoto kutokwenda shuleni.

Lindi. Kukithiri kwa michezo ya kubahatisha katika Manispaa ya Lindi kumetajwa kuwa chanzo cha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutokwenda shule.

Kutokana na changamoto hiyo, Baraza la Madiwani wamemtaka mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo kuhakikisha michezo hiyo inaondolewa kwenye manispaa yao.

Akizungumza wakati wa maswali na majibu ya papo kwa hapo leo Novemba 9, Diwani wa Kata ya Kilangala Kassim Namwete amesema kuwa kwenye kata yake wanafunzi hawendi shule badala yake wanashinda kwenye michezo hiyo ya kubahatisha. 

Ameendelea kusema kuwa, michezo ya kubahatisha kwenye kata yake inachangia kupoteza nguvu kazi kwa vijana pamoja na wanafunzi kutokwenda shuleni na kuchangia kudhorotesha uchumi wa kata na mkoa kwa ujumla.

“Mimi kama diwani sitaki kuona mchezo wa kubahatisha kwenye kata yangu, siupendi kabisa kwa kuwa unasababisha watoto wetu kutokwenda shule pamoja na vijana kushindwa kufanya kazi na kuendekeza michezo hiyo,” amesema Namwete

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Msinjahili, Asina Kawanga amesema kuwa michezo ya kubahatisha si mizuri kwenye jamii kwa kuwa inasababisha watoto walio chini ya miaka 18 kwenda kucheza michezo hiyo wakati wanatakiwa kuwa shule.

"Niwaombe wanawake wenzangu kuwazuia watoto wetu kwenda kucheza michezo hiyo, mtoto anashindwa kwenda shule anakwenda kucheza michezo ya kubahatish,” amesema Asina.

Hata hivyo, akiwajibu madiwani hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele amesema kuwa wenye michezo yote ya kubahatisha wapo kwa mujibu wa sheria na ndio maana kuna bodi ya michezo ya kubahatisha.

"Hawa watu wapo kwa mujibu washeria na pia sisi manispaa hatuwezi kuchukua jukumu la moja kwa moja kuwafukuza kwakuwa na wao pia wanachangia pato kwa Halmashauri yetu," amesema Mnwele.

Lakini baadhi ya wakazi wa Lindi hawajaridhishwa na michezo hiyo, akiwamo Zaituni Jumbe aliyesema vijana pamoja na watoto hawafanyi kazi na hawaendi shule kwa kuwa wanajua wanapata hela.

"Niiombe Serikali ya Wilaya kuweka utaratibu wa hii michezo ianze kuchezwa saa ngapi na iwekwe kwenye maeneo husika kama kwenye kumbi za starehe, lakini sio kuwekwa kiholela," amesema Zaituni.