Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mafuta ya kula kutoka nje yashusha bei ya alizeti Singida

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo alipokelewa na wanachama wa CCM katika kijiji cha Iguguno kilichopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake.

Mkalama. Mafuta ya kula yanayoingizwa nchini yameshusha bei ya alizeti mkoani Singida, jambo linalodaiwa kuwakatisha tamaa wakulima wanaozakisha zao hilo mkoni humo.

Hayo yamebainishwa leo Machi 2, 2023 na Mbunge wa Mkalama, Francis Isaack wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo katika Wilaya ya Mkalama kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020.

Akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika katika shina namba tano lililopo katika Kata ya Iguguno, Isaack amesema bei ya alizeti imeshuka, haiendani na gharama za uzalishaji.

Amesema kitu kilichosababisha hali hiyo ni mafuta ya kula kuingizwa nchini bila kodi, jambo ambalo limesababisha mafuta ya ndani kushindwa kushinana na mafuta hayo sokoni.

"Ndugu Katibu Mkuu, nikuombe utete na Mama (Rais Samia Suluhu Hassan), angalau hata kama yanaingiza kutoka nje basi na haya ya alizeti yanunuliwe pia.

"Wakulima wengi wamevunjika moyo wa kulima alizeti kwa sababu msimu uliopita hawajauza alizeti zao, bado zimejaa kwenye maghala kwa sababu bei iko chini sana," amesema Isaack.

Akisisitiza jambo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kurudisha kodi ya mafuta ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi.

"Tukiweka kodi, maana yake tutaweza kushindana, alizeti zetu zitapanda bei," amesema Serukamba wakati akizungumza kwenye mkutano huo.

Ameongeza kwamba serikali imehamasisha wananchi kulima, imetoa ruzuku ya pembejeo na mikopo ya mbegu, lakini wanakatishwa tamaa na hali ya bei ya alizeti ambayo haiendani na gharama za uzalishaji.

Serukamba amesema Singida wamelima ekari 600,000 za alizeti, maana yake zikivunwa, asilimia 44 ya mafuta ya kula nchini yatatoka mkoani humo.

Akizungumzia hoja hiyo, Chongolo amesema amelichukua, atakwenda kujadiliana na wenzake kuona namna bora ya kulitatua ili wakulima waendelee kuzalisha kwa faida.

"Tumehamasishana kulima, tumelima. Hatuwezi kuhamasisha wawekezaji wa nje wakati wa ndani hawanufaiki. Hili nimelibeba, ngoja tukajadiliane na wenzangu huko," amesema Chongolo huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.