Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magufuli aeleza Channel 10 ilivyorejeshwa CCM

Magufuli aeleza Channel 10 ilivyorejeshwa CCM

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania,  John Magufuli amesema amefurahishwa vyombo vya hahari ya Channet 10 na Magic FM kurejeshwa mikononi mwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania,  John Magufuli amesema amefurahishwa vyombo vya hahari ya Channet T10 na Magic FM kurejeshwa mikononi mwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema ufisadi ndani ya chama hicho tawala uliokuwa umeota mizizi na ulididimiza chombo hicho.

Magufuli ameyasema hayo leo Alhamisi Februari 25, 2020 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya siku tatu jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahi sana kuona Tv zetu, vyombo hivi vilikuwa ni vya chama cha mapinduzi katikati Channel 10 ikachukuliwa na kuwa mali ya watu wengine tulinyang’anywa na kudhulumiwa, namshuru Bashiru (Ally- katibu wa CCM).”

“Nilipounda tume ya kuchunguza mali za chama cha mapinduzi ndiyo akaja na  tukairudisha Channel 10 ikawa yetu na mnaona mambo mengi yanafanyika na namna gani ufisadi ulikuwa umeota mizizi na hata mali nyingine zilikuwa zinapotea bila habari,” amesema Rais Magufuli akibainisha kuwa zaidi ya miaka 16 jengo hilo lilikuwa kama gofu.

Akiwashukuru wafanyakazi amesema, “wafanyakazi mmefanya kazi katika mazingira magumu lakini mmevumilia ninaona mambo mazuri sana mmeijenga historia ya Tanzania hapa ndiyo chuo kikuu cha Dar es Salaam kilipoanzishwa wengi hawajui ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza historia ya nchi yetu.”