Mahabusu 20 watoroka kituo cha polisi

Kizaazaa polisi mahabusu wakitoroka

Muktasari:

  • Polisi wadai mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo.

Dar es Salaam. Mahabusu zaidi ya 20 waliokuwa wanashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, kilichopo Mbagala wilayani Temeke wametoroka baada ya kumpiga askari kisha kuvunja lango la chumba cha mahabusu na kutokomea kusikojulikana.

 Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, jijini Dar es Salaam limethibitishwa na Jeshi la Polisi huku likisema wanaendelea na msako wa kuwabaini walipo mahabusu hao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo alipotafutwa na Mwananchi azungumzie tukio hilo, alisema yuko msibani Kibondo, atafutwe kaimu wake, Daniel Shila ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda ya Maalum Dar es Salaam azungumzie hilo.

Kamanda Shila alipotafutwa na Mwananchi alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema “waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo, si wale wenye kesi mbalimbali.”

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la Mwananchi leo.