Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yapokea vielelezo vinne kesi mauaji ya Masumbuko

Zephania Ndalawa anayetuhumiwa kumuua Thomas Masumbuko akiwa kwenye chumba cha Mahakama muda mfupi kabla kesi kuanza.

Muktasari:

  • Shahidi huyo ameeleza pia alishuhudia mwili wa marehemu ukiwa umeshindiliwa matambara mdomoni, huku mtu mwingine akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa na shoka kichwani na pembeni kukiwa na shoka lenye damu.

Geita. Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Geita, imepokea vielelezo vinne vilivyotolewa na upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili Zephania Ndalawa anayeshtakiwa kwa kosa la kumuua Thomas Masumbuko.

Katika kesi hiyo iliyoko chini ya Jaji Graffin Mwakapeje vielelezo vilivyopokelewa mahakamani hapo ni pamoja na hati ya dharura ya upekuzi, shoka lililotumika kumjeruhi mtu lililotolewa na askari eneo la tukio.

Kilelezo kingine ni pamoja na hati ya fomu ya dharura ya kupokwa pikipiki na kielelzo cha nne ni pikipiki aliyokuwa akiiendesha mshtakiwa yenye namba MC 154 DJV aina ya SanLG.

Akiongozwa na Mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Musa Mlawa, shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ambaye ni Askari Mpelelezi  na Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kakubiro, Shaban Shaban ameieleza mahakama kuwa Agosti 19,2023 akiwa kazini Kakubiro alipata taarifa kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Senga akimueleza kuna tukio la mauaji kwenye eneo lake.

“Alinieleza kwenye eneo lake kuna mauaji ya mtoto aliyewekewa tambara mdomoni na kukosa hewa hivyo kufariki na baada ya kupokea taarifa hiyo nilimpigia simu Mkuu wa polisi Geita kumpa taarifa na  yeye aliniambia nitangulie anakuja na timu ya makachero,“ ameeleza Sajenti Shaban.

Amedai baada ya kufika eneo la tukio na kukagua kwenye chumba kimoja alikuta alimkuta majeruhi aliyekuwa amejeruhiwa kwa kukatwa shoka pamoja na shoka lenye damu lililotumika kumjerehi.

Shahidi huyo ameeleza pia alishuhudia mwili wa marehemu uliokuwa umeshindiliwa matambara mdomoni ukifanyiwa uchunguzi na daktari.

Amedai katika mahojiano watu wawili wa familia hiyo walimueleza kuwa mtu aliyekuja kufanya tukio hilo ni mtu anaefanya kazi ya kubeba mazao shambani wakati wa msimu wa mavuno  waliyemtaja kwa jina moja la Zephania Ndalawa aliyekuwa dereva bodaboda.

Shahidi wa pili Lufungulo Ndelema ameieleza Mahakama kuwa Ogosti 19, 2023 akitoka nyumbani kwake kuelekea kwa mama yake aitwae Salome Lufungulo akiwa njiani alikutana na pikipiki ikiendeshwa  na dereva pamoja na mtu mwingine nyuma ikitoka nyumbani kwa mama yake ikiwa na gunia la mahindi pamoja na runinga.

“Nilisimamisha pikipiki na kuhoji kuhusu TV maana niliona inafanana na ya dada yangu, ndipo aliyekuwa nyuma alishuka na kunikaba nikaanguka wakaanza kunipiga kwenye miguu baadaye wakanipeleka ndani na kunifunga mikono na miguu na kunikata na shoka kwenye kichwa,” amedai.

Ameendelea kudai kuwa akiwa hospitali alielezwa na ndugu yake kuwa watu hao wamemuua mtoto wa dada yake.

Akiulizwa maswali ya dodoso na wakili wa utetezi Beatrice Amos kuhusu jina la mtoto wa dada yake aliyefariki alidai hamkumbuki.

Wakili huyo alimuhoji pia kuhusu umbali wa majirani na nyumba ya nyumba ya mama yake na kudai ni kama umbali wa hatua 10 na kuulizwa kama alipiga kelele wakati anapigwa na kudai hakupiga kelele.

Kesi hiyo bado inaendelea mahakamani ambapo shahidi wa tatu anatoa ushahidi.