Maimu, wenzake wasomewa mashtaka 100

Muktasari:
- Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na wenzake watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka mapya 100, yakiwamo ya kufanya udanganyifu
Dar es Salam. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na wenzake watano, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kijibu mashtaka mapya 100, yakiwamo ya kufanya udanganyifu.
Akisoma hati ya mashtaka leo Jumanne Januari 29, 2019, Wakili wa Serikali Simon Wankyo akisaidia na Leoanard Swai mbele ya hakimu Salum Ally, amedai washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 7 /2019.
Washtakiwa wanadaiwa kughushi na kufanya udanganyifu katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), hivyo kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.1 bilioni.
Endelea kufuatilia Mwananchi kujua undani wa mashtaka hayo katika kesi inayoendelea mahakamani hapo