Majangili watatu wanaswa na meno ya tembo

Lindi. Jeshi la polisi mkoani Lindi kwa kushirikia wahifadhi wanyamapori Tawa wamewakama watu watatu kwa kutuhuma za kukutwa na meno tembo mazima 28 na vipande 62.

 Hayo yameelezwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Lindi, ACP Pili Mande wakati akizungumza na wana habari ofisi kwake jana.

Kamanda Mande amesema watuhumiwa waliokamatwa ni Said Seleman Litangulu miaka 55, Selemani Hassan miaka 32 na Bakari Said miaka 22 ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Nanjilinji kilichopo wilayani Kilwa.

Kamanda mande aliongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo  limewakamata watu 122 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukutwa na nyara za serikali kama vile  nyama Nyati, madawa ya kulevya aina bangi, wizi wa mali kama runinga, simu na pikipiki na pombe ya Moshi.

Kwa upande kamishna msaidizi wa uhifadhi kutoka katika Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori (Tawa), Kennedy Sanga amesema meno na vipande hivyo vinaonyesha ni takribani Tembo 30 hali inayoharibu mfumo wa uhifadhi huku akiwataka wakazi kuacha mara moja matukio haya kwani ni makosa ya kiuhujumi uchumi ambapo tayari wameshaandaa mipango kuwadhibiti wanaohusika na ujangili huo.