Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mali makontena ya Makonda zaanza kupigwa mnada

Muktasari:

Mnada huu ni wa makontena 20 yenye samani na ulianza Jumamosi wiki iliyopita.


Dar es Salaam. Mnada wa mali zilizomo ndani ya makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, unaendelea na tayari wateja wameshakagua bidhaa na wanashindana kununua.

Bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela amewataka wanunuzi kuwa na vitambulisho, leseni ya gari na pasi ya kusafiria.

Hata hivyo, bado wateja wengi hawajafikia bei zinazotakiwa.

Bei zinazotajwa ni kati ya Sh6 milioni hadi 15 milioni.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Yono Kevela aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna matumaini ya bidhaa zote kununuliwa tofauti na mnada wa awali uliokosa wateja.

Mnada huo unafanyika katika bandari kavu ya Malawi Cargo.