Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama aliyemchoma mikono mwanaye afungwa jela miaka mitano

Muktasari:

Mkazi wa Kijiji cha Shahende wilayani Geita, Mpipi Emanuel (33) amemhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumchoma mikono mwanaye Helena Bahati na kumsababishia maumivu.

Geita. Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Shahende wilayani Geita, Mpipi Emanuel (33) kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumjeruhi kwa kumchoma mikono, mwanaye Helena Bahati.

Hukumu hiyo katika kesi ya jinai namba 200 ya mwaka 2022 ilitolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Samuel Maweda.

Amesema kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo ni cha kikatili na kimesababisha ndoto ya Helena ya kuhitimu darasa la saba kutotimia

Awali mwendesha mashtaka wa Serikali, Shukrani Msuya aliieleza mahakama kuwa Oktoba 4, 2022 mshatakiwa alimpiga mtoto huyo na kumchoma moto mikono na kumsababishia maumivu kinyume na sheria.

Mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama imsamehe na kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia ya watoto watano ambao wanamtegemea na kuwa hilo ni kosa lake la kwanza.

Maweda alisema kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ni kinyume na sera ya nchi juu ya elimu kwa watoto wa kike.