Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Massay: Sitapiga tena sarakasi bungeni

Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay akiwa amebinuka sarakasi ndani ya ukumbi wa Bunge alipokuwa akichangia mjadala wa kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jijini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Baada ya Serikali kutia saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kilomita 25 kutoka Labbay hadi Haydom Mbunge wa Mbulu vijijini Mkoani Manyara (CCM), Flatey Massay ameyasema hatapiga tena sarakasi bungeni.

Haydom. Mbunge wa Mbulu Mkoani Manyara, Flatey Massay (CCM) amesema hatapiga tena sarakasi bungeni kudai kujengewa barabara kwani Serikali imeshaanza ujenzi wa barabara ya lami jimboni kwake.

 Ujenzi wa barabara hiyo itahusisha mwendelezo wa kilomita 389 za lami kutoka Karatu mkoani Arusha, kwenda Mbulu na Haydom mkoani Manyara hadi Sibiti, Lalago wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Massay ameyasema hayo leo ijumaa Mei 19 mji mdogo wa Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara, kwenye utiwaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kilomita 25 kutoka Labbay hadi Haydom.

Amesema anaishukuru serikali ya awamu ya sita kuanza ujenzi wa barabara hiyo ina umuhimu mkubwa tangu Mbulu ianzishwe mwaka 1905.

"Jumatatu ijayo mnatarajiwa kusoma bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi jijini Dodoma bungeni kwa mwaka 2023/2024 hivyo sitapiga sarakasi zaidi ya kusema asanteni," amesema Massay.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema kilomita 25 hizo zinakamilisha kilomita 50 kati ya kilomita 113 za Barabara ya Serengeti Southern Bypass zilizopo ndani ya Mkoa wa Manyara.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanrodos), Mhandisi Rogatus Mativila amesema kipande cha kilomita 25 kutoka Labbay hadi Haydom kitagharimu Sh42 billioni.

Mhandisi Mativila amesema ujenzi wa barabara hiyo utahusisha upana wa mita 11 ambapo mita saba za njia ya magari na mita mbili kila upande kwa watembea kwa miguu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara, Peter Toima amesema ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa ilani ya CCM mwaka 2020/2025.

Toima amesema barabara nyingine za mkoa huo zinapaswa kujengwa kwa kiwango cha lami kwani zipo kwenye ilani ikiwemo ya barabara ya kutoka Mbauda jijini Arusha, Orkesumet wilayani Simanjiro, Kibaya wilayani Kiteto hadi Kongwa mkoani Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema Manyara ina changamoto za barabara za lami kuunganisha wilaya zake.

Massay akiwa bungeni Mei 23 mwaka 2022 alipiga sarakasi akidai kuwa barabara hiyo haijengwi ili hali kila mwaka anaisemea na haitengewi fedha za ujenzi.