Mawakili wapya wapewa mbinu

Muktasari:
- Lengo la mafunzo hayo ni yaliyohusisha mawakili wapya 524 ni kuwaanda kuingia sokoni kwa kutoa huduma za kisheria kwa kufuata sheria na miongozi iliyopo.
Dar es Salaam. Mawakili wapya 524 wametakiwa kwenda kutoa huduma za kisheria vijijini ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hao kama migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji, mirathi, ndoa na kuvunjwa kwa haki za binadamu.
Pia, wametakiwa kuchangamkia fursa ya utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa kujiunga na kuwa wanachama wa Jumuiya hiyo ili waweze kukutana na wenzao kutoka katika nchi hizo na kupata fursa zinazojitokeza kwenye mbalimbali.
Hayo yamesemwa Desemba 11, 2024 na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mawakili wa Afrika Mashariki, John Seka wakati akiwajenge uwezo mawakili hao wapya 524.
Amesema kama mawakili wote watakaa mjini, basi watashindwa kupanua wigo wa kutoa huduma za kisheria vijijini.
“Kwa sababu uwakili ni huduma, sasa ili tuweze kujenga huduma hii inabidi tusambaze mikao yote na wilaya zote na ikiwezekana kata zote, hivyo tunataka mawakili waende huko wakatatue changamoto za kisheria kwa wananchi vijiji kwani kuna migogoro ya ardhi, migogoro ya wakulima na wafugaji, miradhi, ndoa, kuvunjwa kwa haki za binadamu, haki za watoto” amesema
Seka ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na wakili wa Mahakama Kuu, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaonyesha fursa ambazo zipo katika tasnia ya sheria, tasnia ya uwakili lakini changamoto zilizopo, miiko na maadili ambayo wakili anatakiwa kuwa nayo na namna anavyotakiwa awe ili aweze kufanya kazi yenye manufaa.
“Kama mnavyofahamu Tanzania ni nchi kubwa sana kuna mikoa na wilaya ambayo haina mawakili wa kutosha, lakini tukumbuke kuwa mahakama zetu na mawakili sasa wanaruhusiwa kuingia hadi katika mahakama za mwanzo kwa hiyo zipo Kata na Tarafa nyingi hapa nchini ambazo hazina mawakili” amesema Seka.
“Kwa sababu ni vijana na bado wana nguvu, muanze kuona na kupanua wigo wa kwenda katika maeneo ambayo yanauhitaji mkubwa, hivyo tu washawishi waende vijijini ambapo huko watasaidia jamii” amesema.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mawakili wa Afrika Mashariki, John Seka akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mawakili wapya 524 hawapo pichani. Picha na Hadija Jumanne
Amesema fursa nyingine iliyopo kwa mawakili hao ni utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo wametakiwa kujiunga na kuwa wanachama wa Jumuiya hiyo ili waweze kukutana na wenzao kutoka katika nchi hizo na kupata fursa zinazojitokeza kwenye mbalimbali.
“Huduma ya kisheria sasa hivi imekuwa pana na watu wanaohitaji huduma hiyo wapo sehemu mbalimbali, lakini kikubwa zaidi ni kujengeana uzoefu wa kuona umuhimu wa kuchangamana na wenzao ili kupata fursa mbalimbali,” alisema.
Alidainisha kuwa taaluma ya uwakili na taalumu ya sheria ni endelevu, hivyo kila wakati wamatakiwa kujengewa uwezo wa kufahamu maeneo mbalimbali.
Ulimwengu tulionayo ni ulimwengu wa kubobe na kuwa mdhamivu katika eneo flani, hivyo ili uweze kuwa mbobevu au mdhamivu sehemu flani ni lazima usome zaidi na upate mafunzo kutoka kwa watu mbalimbali ili uwe bora zaidi kwenye eneo maalumu.
Amebainsha changamo kubwa ambayo mawakili wengi wanalalamika ni ukosefu wa fedha na ili kuepuka hilo ndio maana wanawajenge uwezo wa kuwapa mbinu za kufanya kazi nje ya mjini.
“Na sisi wanasheria wa TLS, tuna miongozo ya namna ya kutoza gharama, kwa hiyo tunawajengea uwezo wanachama wetu waweze kufahamu gharama na kwamba kama wakizangatia gharama ambazo tumejiwekea kama mawakili, basi hakuna ambaye atakufa njaa, kwa sababu huo mkate upo kwa kila mtu” anasema Seka
Alibainisha kuwa changamoto nyingine ni kuwepo kwa mawakili vishoka ambao wanajihusisha na kazi za uwakili na hiyo inatokana na jamii kutokuwa na uelewa wa kujua gharama za tozo na kujikuta wametafuta mawakili vishoka kwa ajili ya kuwasimamia katika masuala ya kisheri.
Wakili, Salha Rashid kutoka TLS, amesema mafunzo hayo wanatoa kwa ajili kujua nini wanatakiwa wafanye na namna chama hicho kinavyofanya kazi.
“Tunawafundisha namna ya kuwa na nidhamu katika taaluma yao na jinsi wanavyotakiwa kuwa wanapohudumia wateja wao na namna ya kujiepusha na vishoka” amesema Rashid.
Mafunzo hayo yametolewa na chama cha TSL na mawakili wabobezi wa sheria wa hapa nchini.
Nancy Munish ni mmoja wa mawakili wapya, amesema kama mawakili wapya wanatakiwa kuwa wazalendo kwa taaluma yao na kuilinda.
Naye, Victor Alexander amesema mafunzo hayo yamewaandaa namna ya kufanya kazi za uwakili na jinsi ya kuwahudumia wateja wanaohitaji huduma za kisheria.