Mbowe katika muonekano tofauti mahakamani
Muktasari:
- Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa takribani miezi minne sasa.
Dar es Salaam. Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu inaendelea katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa takribani miezi minne sasa.
Katika siku za karibuni imeshuhudiwa katika usikilizaji wa shauri hilo zikiibuka kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, na hiyo ni kutokana na upande wa utetezi kupiga maelezo kuwasilishwa mahakama kama kielelezo katika kesi hiyo.
Mwananchi Digital inakuletea habari picha za Mbowe katika siku tofauti alizokuwa akifikishwa mahakamani hapo kusikiliza mashtaka yanayomkabili.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa maarufu kama Adamoo na Mohamed Abdillahi Ling’wenya.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa ndani ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa ndani ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
Soma zaidi:Ushahidi kesi ndogo ya kina Mbowe huu hapa