Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchengerwa atoa maagizo sita kwa halmashauri

Muktasari:

  • Serikali imesaini mkataba wa miradi inatakayoimarisha huduma za barabara, masoko, vituo vya mabasi na daladala, bustani za mapumziko na burudani, mitaro ya maji ya mvua na vivuko vya maji ndani ya halmashauri 12 katika awamu ya kwanza kwa thamani ya Sh27 6bilioni.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo sita huku akitoa tahadhari ya kuwaondoa madarakani wakurugenzi wote watakaoshindwa kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na utamaduni wa kukaa na fedha hizo bila kuzitumia.  

 Mchengerwa amesema inashangaza mkurugenzi wa halmashauri aliyeaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, akikabidhiwa gari na nyumba lakini anashiriki mtandao wa kuiba fedha za umma.

Aidha, wengine kutotekeleza miradi licha ya kuwa na fedha kwenye akaunti. “Fedha zipo lakini hautumii, sitakubali katika uongozi wangu, nakuhakikishia hautakuwa sehemu ya uongozi wa Serikali hii, sitaacha kuchukulia hatua, nitakusimamisha,” amesema Mchengerwa.

Ametoa kauli hiyo wakati wa utiaji saini mkataba wa miradi itakayoimarisha huduma za barabara, masoko, vituo vya mabasi na daladala, bustani za mapumziko na burudani, mitaro ya maji ya mvua na vivuko vya maji ndani ya halmashauri 12 za miji katika awamu ya kwanza kwa thamani ya Sh276 bilioni.

Halmashauri hizo za majiji, manispaa na miji ni Arusha, Dodoma, Geita, Ilemela, Kahama, Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Songea, Sumbawanga na Tabora, zenye idadi ya watu wanaozidi 250,000. 

Kundi hilo kati ya makundi matatu litahusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 14,754 pamoja na mitandao ya mitaro 24.66 km Dodoma, Kigoma, Kahama, Morogoro na Mbeya.

Mkataba huo ni sehemu ya Mradi ya uboreshaji miundombinu ya miji Tanzania (TACTIC) utakaotekelezwa kwa miaka sita kwa mkopo wa Dola za Kimarekani 410 milioni (Sh984 bilioni kwa sasa) kutoka Benki ya Dunia.

Tukio hilo la utiaji saini chini ya wizara ya Tamisemi limehusisha pande mbili za wakurugenzi wa halmashauri husika, wamasheria wa halmashauri husika pamoja, wakandarasi wa mradi na washauri elekezi wa mradi.


Maelekezo sita

Maelekezo ya Mchengerwa kwa viongozi wa halmashauri hizo ni kusimamia miradi hiyo ikamilike kwa wakati, kulipa fidia ili kuepuka ucheleweshaji miradi na kuongeza ubunifu wa vyanzo vya mapato hususani hoteli pembezoni mwa bahari na maziwa.

Agizo lingine ni kuzuia Kampuni ya Nyanza Roads Limited iliyosaini leo, isikabidhiwe miradi mingine mipya kabla ya kumaliza mradi iliyokadhibiwa na Serikali bila kuona utekelezaji wake huku mwakilishi wa kampuni hiyo akikataa kuzungumza lolote kwa madai ya kutokuwa msemaji.

Hata hivyo kampuni hiyo leo imesaini mradi wa ujenzi wa barabara zenye mtandao wa kilometa 12.8 katika halamshauri ya mji wa Ilemela utakaogharimu Sh23.45 bilioni.

Tano, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) imeagizwa kusimamia barabara na madaraja yote kwa miradi ijayo huku wakiepuka uchimbaji wa mashimo bila kuwa na bajeti. 

“Tarura chimbeni mashimo barabarani mkiwa na bajeti, unachimba yanakaa muda mrefu matokeo yake mnasababisha ajali na magari ya watu kuharibika, nikikuta mashimo hujaendeleza chochote ndani ya wiki mbili unaondoka, nilimuondoa meneja wa Kinondoni,” amesema Mchengerwa.

Sita ni agizo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo kuanza uchunguzi wa watumishi wanaohusika katika mtandao wa wizi wa fedha za umma katika halmashauri tano alizotilia shaka chini ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


Makundi mawili

Katika hatua nyingine, Mratibu wa miradi ya Benki ya Dunia upande wa Tamisemi, Humphrey Kanyenye amesema kundi la pili miji 15 pamoja na miji 18 katika kundi la tatu itatekelezwa katika mwaka 2024/25. 

Wanufaika ni Korogwe, Lindi, Moshi, Mpanda, Mtwara, Musoma, Njombe, Singinda, Shinyanga, Tanga, Bagamoyo, Bunda, Chato, Handeni, Ifakara, Kasulu, Kondoa, Mafinga, Makambako, Masasi, Mbinga, Mbulu, Nanyamba, Newal, Nzega, Tarime, Tunduma Babati, Bariadi, Bukoba, Iringa, Kibaha na Vwawa.

Kwa ujumla yote katika halmashauri 45, itafikia zaidi ya watanzania milioni 10.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, mradi huo unahusisha miundombinu ya barabara za lami, masoko, vituo vya mabasi na daladala, bustani za mapumziko na burudani, mitaro ya maji ya mvua na vivuko vya maji.

Mradi huo unahusisha pia kujenga uwezo kwa watumishi katika halmashauri hizo wa uandaaji wa mipango kabambe kwa vijiji 19, uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji mapato ununuzi wa vitendea kazi na mafunzo ya kuongeza uwezo kwa watumishi wa umma katika halmashauri za majiji, manispaa na miji

Katika eneo la miradi yote ya vituo vya mabasi, masoko, maghala ya kuhifadhia nafaka na bustani, zabuni zitatangazwa mwezi huu wa Septemba kabla ya kuanza kazi Desemba mwaka huu.