Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgodi Buzwagi wapunguza mapato ya Kahama kwa Sh300 milioni

Muktasari:

Mapato ya maji kwenye mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira yameshuka kwa asilimia 50 baada ya mgodi wa Buzwagi kusitisha matumizi ya maji kutoka mamlaka hiyo

Kahama. Mapato ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama mkoani Shinyanga, (Kuwasa) yameshuka kutoka Sh600 milioni hadi Sh300 milioni kwa mwezi baada ya Mgodi wa Buzwagi kusitisha matumizi ya maji kutoka taasisi hiyo.

Hali hiyo ilielezwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo meja mstaafu Bahati Matala wakati akifungua kikao cha baraza la tatu la wafanyakazi katika mamlaka hiyo.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo Jumatatu Novemba 12, 2018 mjini Kahama, Matala amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa bidii na kuongeza wateja zaidi watakaoziba pengo la mapato lililoachwa na Mgodi wa Buzwagi.             

Awali, mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Joel Lugemanila amesema Mgodi wa Buzwagi ulikuwa ukichangia asilimia 50 ya mapato kwa mwezi sawa na Sh300 milioni kati ya makusanyo ya Sh600 milioni.                         

Lugemanila amesema baada ya Buzwagi kusitisha huduma, makusanyo ya sasa ni Sh300 milioni ingawa waliwabembeleza mgodi huo ambao sasa wanachukua maji kidogo ya Sh61 milioni kwa mwezi.                 

Mgodi wa Buzwagi umepunguza matumizi ya maji baada ya kuanza maandalizi ya kufunga mgodi hali iliyochangia kupungua kwa shughuli nyingi za uzalishaji zinazotumia maji.               

Mmoja wa wafanyakazi katika mamlaka hiyo, Magige Marwa amesema pamoja na kupungua kwa mapato hayo lakini watajitahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wateja wao hali itakayoongeza wateja na mapato.

Kuhusu kuzinduliwa kwa baraza la wafanyakazi, Marwa amesema ni sehemu mojawapo itakayokuwa inawaunganisha kupitia chombo hicho ambacho ni sehemu ya kumalizika matatizo yao.