Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlinzi wa shule auawa, wauwaji wabeba kichwa

Muktasari:

  • Mlinzi wa shule ya Winnings Spirit iliyopo eneo la Terati jijini Arusha, Issa Dinaiah (57) amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa huku kichwa kikiwa hakipo.

Arusha. Mlinzi wa shule ya Winnings Spirit iliyopo eneo la Terati jijini Arusha, Issa Dinaiah (57) amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa huku kichwa kikiwa hakipo.

 Mwili wa mlinzi huyo umekutwa leo Jumatano Februari 2, 2022 asubuhi na wafanyakazi wa shule hiyo inayomilikiwa na Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meya Iranghe amesema alipata taarifa za kifo cha mfanyakazi wake mmoja leo asubuhi na baada ya kufika eneo la tukio aliwakuta Polisi.

Iranghe amesema bado chanzo na waliofanya mauaji haya hawajajulikana.

"Naomba kuwasiliana na Polisi ambao ndio wanaendelea na uchunguzi wa tukio hili mimi nimepigiwa simu na wafanyakazi na nimekuta tayari polisi wapo hapa" amesema

Maofisa wa Jeshi la Polisi waliokuwa katika eneo la tukio wameeleza taarifa rasmi itatolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

"Ni kweli tukio limetokea lakini msemaji ni Kamanda wa Polisi Mkoa atatoa taarifa rasmi "amesema mmoja wa maofisa wa Jeshi hilo ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Mary Kupesha hakupatikana kutoa taarifa ya tukio hilo.