Mungereza alikwenda Dodoma kushiriki kikao cha Wizara ya Habari

Friday December 25 2020
ujumbepic

katibu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza

By Kelvin Kagambo

Dar es Salaam. Kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Matiko Mniko ameieleza  Mwananchi Digital  kuwa katibu wa baraza hilo, Godfrey Mngereza alifariki dunia mjini Dodoma alikokwenda kushiriki kikao cha mipango na fedha cha Wizara ya Habari.

Taarifa za kifo cha Mungereza zilitolewa jana  saa 5 usiku zikieleza kuwa kiongozi huyo alifariki akiwa Dodoma.

"Alikwenda Dodoma kwenye kikao. Na jana Alhamisi alihudhuria kikao lakini alipotoka akawa anajisikia vibaya. Akaenda hospitali akapewa matibabu lakini baadaye umauti ukamkuta, " amesema Matiko.

Matiko amebainisha kuwa taarifa zaidi  zitatolewa baadaye.

"Kuhusu alikuwa anasumbuliwa na nini, atazikwa wapi na taarifa nyingine tusubiri majibu kutoka kwa familia. Wamekaa kikao. Tutawajulisha, " amesisitiza.

Advertisement