Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua kubwa yaja, kunyesha mikoa 14 Tanzania

Muktasari:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari  ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tanga , Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Zanzibar.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari  ya vipindi vifupi vya mvua kubwa katika Mikoa 14 nchini.

Mikoa hiyo ni  Dar es Salaam, Pwani, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tanga , Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na kisiwani Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo inaeleza kuwa kuna uwezekano wa kutokea vimbunga pacha Magharibi mwa bahari ya Hindi upande wa Kaskazini na Kusini mwa Ikweta na kuathiri mfumo wa hali ya hewa nchini.

Inaeleza kuwa migandamizo hiyo midogo pacha inaelekea kuimarika na kuwa vimbunga katika pwani ya Somalia (upande wa Kaskazini mwa Ikweta) na Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madagascar (Kusini mwa Ikweta).

Pia,  mgandamizo mdogo wa hewa uliopo Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (karibu na kisiwa cha Madagasca) inatarajia kuimarika na kuelekea Kaskazini mwa kisiwa hicho.

Inaeleza kuwa hali hiyo itasababisha ongezeko la mvua pamoja na vipindi vya mvua kubwa  katika baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini mwa Tanzania kati ya Desemba 5 na 6, 2019.

Kwa upande mwingine mgandamizo mdogo wa hewa katika Pwani ya Somalia unatarajiwa kuendelea kuwa mbali na Pwani ya Tanzania na hautarajiwi kuwa na madhara nchini.