Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yaua mwanafunzi wilayani Same

Muktasari:

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kibacha wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro, Happiness Philipo amefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akivuka mto uliojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Same. Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Kibacha wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro, Happiness Philipo amefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akivuka mto uliojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 19, 2019 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema tukio hilo limetokea jana wakati mwanafunzi huyo akivuka mto huo kwenda nyumbani.

"Ni kweli amefariki baada ya kusombwa na maji  wakati akijaribu kuvuka mto  kuelekea kwenye makazi yao jana jioni,” amesema Hamduni.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema baada ya mtoto huyo kusombwa na maji jitihada  zilifanyika na mwili wake uliokotwa maeneo ya Kishaa.

"Ni habari za kusikitisha kwa kweli kwa mwanafunzi kusombwa na maji, taratibu zinaendelea atazikwa kesho Jumapili,” amesema.