Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanamke uawa kwa kukatwa mapanga nyumbani kwake

Muktasari:

  • Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumkata mapanga mkazi wa Kijiji cha Mwamalulu wilayani hapa, Nshoma Moshi (50), wakati akimwogesha mjukuu wake nyumbani kwake, sababu ikitajwa kuwa ni ugomvi wa mashamba.

Shinyanga. Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumkata mapanga mkazi wa Kijiji cha Mwamalulu wilayani hapa, Nshoma Moshi (50), wakati akimwogesha mjukuu wake nyumbani kwake, sababu ikitajwa kuwa ni ugomvi wa mashamba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 31, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa mashamba baada ya mwanamke huyo kushinda kesi mahakamani na kukabidhiwa mashamba yake.

Kamanda Magomi amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi, ili kuondokana na matukio ya kusababisha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia ambayo yangemalizwa kwa kushirikisha vyombo husika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamalulu, Senga Shimba amesema matukio ya mauaji kuanza kutokea katika kijiji hicho yamewashitua na ameliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliomuua mama huyo kwakumkata mapanga.

Katika tukio jingine, mtu aliyefahamika kwa jina la Willison Jogoo mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Kijiji cha Chembeli Kata ya Didia ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuiba kuku kijijini hummo.