Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndege yateketea kwa moto, yajeruhi

Muktasari:

Ndege hiyo ilianguka baada ya kupata hitilafu na  kisha kuteketea kwa moto wakati inaruka  katika uwanja wa Sasakwa wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara.

Serengeti. Ndege iliyokuwa imebeba watalii watano Raia wa Marekani imeanguka na kujeruhi marubani wawili.

Ndege hiyo ilianguka baada ya kupata hitilafu na  kisha kuteketea kwa moto wakati inaruka  katika uwanja wa Sasakwa wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Januari 2 mwaka huu na kusema kuwa  ndege hiyo aina ya CESNA F.406 Mali ya Air Excell ilikuwa ikiongozwa rubani Mohammed Selemani akisaidiwa na rubani Fahd Salehe.

Kamanda Ng’hazi amesema   ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 12 siku ya tukio  ilikuwa na abiria watano walionusurika, Greg Martin Perelman(60), Susan Perelman(52), Sara Melissa Perelman (23), Danielle Jaffe Perelman(21), Emma Stephanie Perelman(19), ambao ni  familia moja toka nchini Marekani.