Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndejembi achangisha Sh360 milioni ujenzi shule ya yatima

Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratias Ndejembi akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Watoto wanaoishi yatima, mazingira magumu na waliofanyika ukatili wa kijinsia katika kituo cha Huruma Center, kilicho chini ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa.

Muktasari:

  • Ndejembi achangisha Sh360 milioni ujenzi wa shule ya yatima na wanaoishi Huruma Center.
  • Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratias Ndejembi amechangisha Sh360 milioni kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Watoto ya Huruma Center ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa.

Iringa. Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratias Ndejembi amechangisha zaidi ya Sh300 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya watoto yatima, mazingira magumu na waliofanyiwa ukatili kijinsia katika Kituo cha Huruma Center kinachomililiwa na Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa.

Huruma Center ni kituo ambacho pia kumekuwa kikipokea watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti kwenye jamii wanazoishi.

Kulingana na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Iringa wapo watoto ambao imekuwa vigumu kusoma shule za kawaida baada ya kuathirika kisaikolojia kutokana na ukatili waliofanyiwa.

Akiendesha harambee hiyo, Ndejembi ambaye alimuwakilisha Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema licha ya Serikali kuwekeza katika ujenzi wa madarasa na shule mpya, bado upo umuhimu wa shule maalumu.

"Tumewaona hawa watoto, wameimba wimbo ambao ujumbe umetugusa, ni jukumu letu kuwasaidia na kuwafanya waishi vizuri kama watoto wetu," amesema Ndejembi.

Askofu Blaston Gaville amesema watoto wanapaswa kulindwa hivyo wameamua kuwajengea shule ili wasome mazingira wanayoishi.

"Shule hii itakuwa jumuishi, tutapokea na watoto walio kwenye jamii lengo kubwa ni hawa walio kwenye kituo walindwe na kusaidiwa kisaikolojia ili wafikie ndoto zao," amesema Askofu Gaville.

Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Profesa Owdernburg Mdegella amesema ifike hatua jamii iseme basi kuhusu ukatili kwa watoto.

"Hili ni jukumu letu viongozi wa dini tuisaidie jamii, huu ukatili unaoendelea lazima tuhakilishe tunakemea," amesema Mdegella.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema alishaongea na watoto walio kwenye kituo hicho na kujua changamoto walizopitia ambazo zinawafanya wasaidiwe kutimiza ndoto zao.