Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nida yaja na mfumo kujisajili vitambulisho mtandaoni

Muktasari:

Katika kukabiliana na msongamano wa watu katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (Nida), imeanzisha mfumo maalumu ambao utawawezesha wanaohitaji vitambulisho kujisajili kwenye mtandao.

Dar es Salaam. Katika kukabiliana na msongamano wa watu katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa (Nida), imeanzisha mfumo maalumu ambao utawawezesha wanaohitaji vitambulisho kujisajili kwenye mtandao.

Mfumo huo unaotarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi ujao ni kati ya mifumo 14 iliyotengenezwa na watalaamu wa ndani ya mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya sita ikilenga kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.

Msemaji wa mamlaka hiyo, Geofrey Tengeneza amesema mfumo huo tayari umeshafanyiwa majaribio na utapelekwa kwa wananchi Aprili mwaka huu ili uanze kutumika kuwarahisishia katika hatua za mwanzo za usajili.

Amesema, “Kupitia mfumo huu mwananchi anayehitaji kitambulisho ataweza kujaza taarifa zake zote zinazohitajika katika hatua za awali, atakwenda kwenye ofisi za Nida pale tu atakapotakiwa kwenda kukamilisha usajili kwa hatua za kuweka alama za vidole na kupiga picha.

“Hii yote ni matokeo ya uwezekezaji mkubwa na maboresho yaliyofanyika ndani ya mwaka mmoja ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita ambayo inalenga kuwasogezea wananchi huduma na kutaka ufanisi kwenye uendeshaji wa shughuli zake,”.

Pamoja na hilo Tengeneza amesema katika kipindi hicho cha mwaka mmoja Nida imeweza kuunganisha wilaya tano katika kituo cha kuchakata taarifa na kufanya jumla ya wilaya 133 kuwa kwenye kituo hicho kati ya wilaya 150.

Amezitaja wilaya hizo mpya zilizoingia kwenye kituo cha kuchataka taarifa ni Siha, Sikonge, Mlele, Wanging’ombe na Kalambo huku Kyerwa na Nyang’wale zikiendelea na majaribio.

Pia ndani ya mwaka mmoja wameunganisha wadau 52 kwenye kanzidata ya utambulisho ya mamlaka ambao wapo kwenye mfumo wa uushirikishwaji wa taarifa.

“Kuunganishwa huko kunafanya jumla ya taasisi 58 zilizotumia mfumo wa Nida kati ya hizo 25 za serikali na 32 taasisi binafsi. Hii inahusisha taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi. Mamlaka yetu ndiyo yenye taarifa za wananchi zenye kuaminika, hapa wanaweza kupata taarifa za uhakika. Lengo ni kuwahudumia wananchi kwa haraka na urahisi huku hao watoa huduma wakabaki na taarifa za uhakika za waliyemhudumia, " amesema Tengeneza.