Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polepole afafanua kuhusu ‘wahuni’

Muktasari:

  • Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amefafanua kauli yake kuhusu neno ‘wahuni’

Dar es Salaam. Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole amefafanua kauli yake kuhusu neno ‘wahuni’ akisema amelitumia kuwakilisha watu wanaotanguliza maslahi yao mbele badala ya maslahi mapana ya  taifa.

Polepole ameyasema hayo leo Desemba 11, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu msimu wa pili wa kipindi chake cha Shule ya Uongozi ambacho maudhui yake hurushwa mtandaoni.

Amesema kauli hiyo imetokana na namna alivyokuwa akifundisha katika kipindi chake kuhusu maslahi ya taifa.

“Ni kwamba tusipokuwa makini wahuni wapo wa kidunia, kimataifa watakuja hapa watapiga kopi serikali yetu, naipenda nchi yangu nimezaliwa hapa na hata siku ya mwisho nitaondokea hapahapa.

“Ni wajibu wetu kukumbushana na kusaidiana maarifa. Kuna mgongano wa kimaslahi, maslahi ya taifa na mtu mmoja mmoja siku zote maslahi huwa ya makundi matatu. Maslahi ya taifa, makundi na maslahi ya mtu mmoja mmoja,” amesema.

Polepole aliyewahi kuwa Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema mara nyingi maslahi ya mtu mmoja huja kwanza na kisha maslahi ya makundi yanafuata.

Alisema kuna watu ambao maslahi ya taifa wanayaweka kando au mwishoni na wanaopanga hivyo ni wahuni, “Neno wahuni sijaanza nalo leo, wahuni wanaopenda maslahi binafsi kwanza wapo.

“Mhuni ni mhuni tu hawabadiliki, nitoe rai kwa viongozi wawe macho na wahuni, awamu jana alitukana Serikali leo anakaa upande wa Serikali.

“Na hili la wahuni nililizungumza sana ni wale wanakwepa kodi utawapata ukienda TRA, wabadhirifu wa mali za umma wapo nenda Takukuru utawakuta, kazi yetu kama viongozi wa taifa ni kuwadhibiti.

“Sasa naongea mtu mwingine anaibuka. Hivi mimi niite wahuni halafu mtu na akili zake timamu anasimama na kujijumuisha au kufurahia? Niseme wazi watu wakizingua mahala natoka tena nazungumza. Nitatumia kila fursa kuhakikisha na mimi natumia nafasi yangu kushughulika na wahuni,” amesema Polepole.